Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI nyota na tegemeo Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba wanakwenda Zimbabwe si kupigania sare, bali kupata ushindi mwingine dhidi ya wenyeji, FC Platinum.
Kikosi cha wachezaji 18 wa Yanga SC kinaondoka asubuhi ya leo Dar es Salaam kwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika na Ngassa amesema wanakwenda kushinda.
Platinum wanatakiwa kushinda mabao 4-0 Uwanja wa Mandava kesho ili kwenda 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, baada ya awali timu hiyo yenye maskani yake Zvishavane kufungwa mabao 5-1 Dar es Salaam, lakini Ngassa amewaambia “Msijidanganye”.
“Sisi tunakwenda Zimbabwe si kwa ajili ya kupigania sare, tunakwenda kule kucheza kwa kushambulia kuanzia mwanzo ili tufunge mabao. Na tutawafunga. Kama unaongoza mabao 5-1, huwezi kupaki basi, sisi tunakwenda kuwashambulia na tutawafunga, ila sidhani kama itakuwa tano tena,”amesema Ngassa.
Mfungaji huyo bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, amesema kwamba Platinum si timu ya kuwatisha tena baada ya kuuona mchezo wao na kuusoma vizuri katika mechi ya kwanza hapa Dar es Salaam.
“Jamaa wana ukuta mwepesi sana ambao hauwezi kuizuia fowadi ya Yanga kufunga japo mabao mawili popote pale ndani ya dakika 90. Tunakwenda Zimbabwe kwa matumaini makubwa kabisa,”amesema Ngassa.
Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka leo ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
Viungo ni Salum Telela, Said Juma, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na washambuliaji Danny Mrwanda, Amisi Tambwe na Hussein Javu.
Benchi la Ufundi litaongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Sufiani Juma, mtunza vifaa, Mahmoud Omar ‘Mpogolo’ na Mchua misuli Jacob Onyango.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kuanzia Saa 4:00 asubuhi kwa ndege maalum ya kukodi ya serikali na itafikia katika hoteli ya Rainbow na jioni itakwenda kufanya mazoezi ya kuuzoea Uwanja wa Mandava, umbali wa kilomita 200.

![]() |
| Mrisho Ngassa kulia amesema kwamba wanakwenda Zimbabwe kushinda |

.png)
0 comments:
Post a Comment