MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amepona maumivu ya goti na yuko tayari kucheza Jumapili mechi ya La Liga dhidi ya Celta Vigo.
Nyota huyo wa Argentina alikuwa nje katika mechi zote za kirafiki za kimataifa, dhidi ya El Salvador na Ecuador, lakini baada ya kurejea Barcelona Alhamisi, alikuwa tayari kufanya mazoezi mepesi kama kukimbia na kunyoosha viungo.
Messi anatarajiwa kuwa fiti kama ambayo taarifa katika tovuti ya klabu yake imesema: "Hali ya goti la Messi imeimarika na mchezaji huyo anatarajiwa kuungana na wenzake waliorejea kutoka kwenye mechi za kimaataifa kesho.'

Lionel Messi akiwapungia mkono mashabiki wakati wa mazoezi mjini Barcelona Alhamisi

Messi alifanya mazoezi mepesi pamoja na Muargentina mwenzake Javier Mascherano baada ya kupona goti
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3023268/Lionel-Messi-recover-foot-injury-make-Barcelona-s-La-Liga-clash-Celta-Vigo.html#ixzz3WBDyhs40


.png)
0 comments:
Post a Comment