• HABARI MPYA

    Tuesday, January 14, 2014

    TAIFA STARS KUIKABILI NAMIBIA FIFA DATE

    Na Boniface Wambura, Ilala
    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.
    Stars na Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
    Taifa Stars

    Makubaliano ya kucheza mechi hiyo yamefikiwa kutokana na mazungumzo kati ya Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA), John Muinjo.
    Benchi la Ufundi la Brave Warriors linaongozwa na kocha mzawa Ricardo Mannetti, na mechi hiyo itachezwa ama Uwanja wa Sam Nujoma au Uwanja wa Uhuru jijini Windhoek.
    Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inafundishwa na kocha Kim Poulsen kutoka Denmark na inatarajia kuanza kucheza mechi za mchujo za AFCON Septemba mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS KUIKABILI NAMIBIA FIFA DATE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top