• HABARI MPYA

    Tuesday, January 21, 2014

    LALA SALAMA VPL YANZA JUMAMOSI YANGA NA ASHANTI DAR, UWANJA WA MBEYA CITY WATIWA KUFULI

    Na Boniface Wambura, Ilala
    MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa Uwanja mwingine.
    Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.
    Wazee wa Uturuki; Yanga wataanza na Ashanti Jumamosi Uwanja wa Taifa
    Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.
    Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa Uwanja mwingine kwa vile huo bado nyasi zake ambazo zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.
    Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta Uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.
    Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LALA SALAMA VPL YANZA JUMAMOSI YANGA NA ASHANTI DAR, UWANJA WA MBEYA CITY WATIWA KUFULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top