• HABARI MPYA

    Monday, January 13, 2014

    MALINZI HAKUNA KULALA TFF, NI KAZI MWANZO MWISHO

    Na Boniface Wambura, Ilala
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafanya ziara ya siku moja kutembelea kituo cha mpira wa miguu wa vijana cha Alliance cha jijini Mwanza.
    Lengo la ziara hiyo ni kuangalia jinsi Alliance inayoendesha shughuli zake ili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liweze kushirikiana na kituo hicho kwa karibu.
    Rais Malinzi katika ziara hiyo atakayoifanya keshokutwa (Januari 15 mwaka huu) atafuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya ya Vijana ya TFF, Ayoub Nyenzi na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ramadhani Nassib.
    Mtu wa kazi; Rais wa TFF, Jamal Malinzi amekuwa akfanya kazi kwa juhudi tangu ameingia madarakani mwishoni mwa mwaka jana

    Alliance inatarajia kufanya mashindano yatakayoshirikisha vituo vyote vya kuendeleza soka kwa vijana (academy) wiki ya tatu ya Februari mwaka huu jijini Mwanza.
    Mashindano hayo yatashirikisha timu za umri wa miaka 13, 15 na 17 ambapo Alliance itagharamia malazi, chakula na usafiri wakati timu hizo zikiwa jijini Mwanza.
    Katika hatua nyingine, TFF imesma imepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Boniface Njohole kilichotokea jana (Januari 12 mwaka huu) mkoani Morogoro.
    Njohole ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Chama cha Soka Morogoro (MRFA) hadi umauti unamkuta anatarajia kuzikwa kesho (Januari 14 mwaka huu) kijijini kwao Mngeta wilayani Ifakara.
    TFF imesema msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani alitoa mchango akiwa mchezaji, kocha na kiongozi kwa nyakati tofauti, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
    TFF imetoa pole kwa familia ya marehemu Njohole, klabu ya Reli na MRFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. 
    Aidha, TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake.
    Wakati huo huo: Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) ya TFF, Hamad Yahya atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa semina ya waamuzi na makamisha.
    Semina hiyo ya siku mbili itafungwa kesho (Januari 14 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Waamuzi zaidi ya 100 na makamishna 50 wanashiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
    Kwa upande wa waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL. TFF inatarajia kuandaa semina nyingine baadaye mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI HAKUNA KULALA TFF, NI KAZI MWANZO MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top