IMEWEKWA JUNI 3, 2013 SAA 10:00 JIONI
KOCHA Jose Mourinho leo amekutana na viongozi wa Chelsea kukamilisha mpango wa kurejea kwake Stamford Bridge.
Taarifa rasmi inatarajiwa kutolewa baadaye leo kuthibitisha kusaini kwake Mkataba wa miaka minne hii ikiwa ni mara ya pili kwa Mourinho kufanya kazi klabu hiyo ya London, kiasi cha saa kadhaa tu tangu aache kazi Real Madrid.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 50 tayari imethibitika ataanza kazi Chelsea wiki hii.

Amerudi England: Jose Mourinho amerejea London tayari kuanza kazi Chelsea

Mourinho alipigwa picha akiwasili Uwanja wa Ndege wa Heathrow jana



.png)