• HABARI MPYA

    Friday, June 28, 2013

    NOTA WAWILI MAKINDA WA TANZANIA WAULA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE

    Katibu wa TFF, Angetile Osiah (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo. Kulia ni Abdulrasul Bitebo na kushoto ni Martine Omella Tegazi
    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JUNI 28, 2013 SAA7:58 MCHANA
    WACHEZAJI wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
    Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.
    Martine Omella

    Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.
    Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
    TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.
    Abdilrasul Bitebo

    Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal, ambacho kuna Mtanzania mmoja, Organes Molel.
    Mwanasoka bora wa dunia, Muargentina Lionel Messi anayechezea Barcelona ya Hispania, jana amefanya ziara katika kituo hicho na kujionea namna nyota wa kesho wanavyoandaliwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NOTA WAWILI MAKINDA WA TANZANIA WAULA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top