• HABARI MPYA

    Thursday, June 27, 2013

    POULINHO AIPELEKA BRAZIL FAINALI KOMBE LA MABARA IKIIUA URUGUAY 2-1, FORLAN AKIKOSA PENALTI

    Paulinho ameibeba Brazil leo

    IMEWEKWA JUNI 27, 2013 SAA 6:37 USIKU
    BAO la kichwa la Paulinho zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho, limeipa Brazil ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay usiku huu na kutinga Fainali ya Kombe la Mabara.
    Diego Forlan alikosa penalti dakika ya 13, baada ya beki wa Chelsea, David Luiz kumuangusha Diego Lugano kwenye eneo la hatari.
    Brazil ilipata bao la kuongoza dakika ya 40, wakati Neymar alipoitokea pasi ndefu ya Paulinho na kuingia ndani kisha kufumua shuti lililombabatiza beki wa Uruguay kabla ya kumkuta Fred, aliyefunga.
    Iliwachukua Uruguay dakika tatu tangu kuanza kipindi cha pili kusawazisha bao hilo, baada ya mabeki wa Brazil kuzembea kuondosha mpira kwenye eneo la hatari wakati pasi hafifu ya Thiago Silva ilipomkuta Edinson Cavani aliyefunga.
    Fainali ya michuano hiyo 'amsha amsha' kuelekea Fainali za Kombe la Dunia, itapigwa mjini Rio de Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana Jumapili.
    Brazil ilibadilisha kikosi kutoka kile kilichoifunga Italia katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A, ikimuanzisha Paulinho badala ya Hernanes katika kiungo.
    Uruguay ilimuacha nje Abel Hernandez, mshambuliaji kinda wa Palermo, ambaye alifunga mabao manne dhidi ya Tahiti katikati ya wiki, na kuwaanzisha kwa pamoja mbele ya mdomo wa goli Luis Suarez, Diego Forlan, na Edinson Cavani.
    Huo ni ushindi wa nne mfululizo kwa Brazil katika michuano ya mwaka huu na wao tano kwa jumla chini ya kocha Luiz Felipe Scolari, kasi ambayo inaweza kuwainua kutoka nafasi ya 22 katika viwango vya FIFA, nafasi ya chini zaidi kwao kuwahi kushika daima.
    Pia unaendeleza rekodi ya kutofungwa na wapinzani wao hao wa Amerika Kusini katika mechi nane sasa tangu Julai 2001.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar/Hernanes dk72, Gustavo, Paulinho, Fred, Hulk/Bernard dk64 na Neymar/Dante dk90.
    Uruguay: Muslera, Lugano, Godin, Caceres, Maxi Pereira, Rodriguez, Arevalo Rios, Gonzalez/Gargano dk83, Forlan, Suarez na Cavani.
    Joy: Brazil booked their place in the final of the Confederations Cup with a 2-1 win over Uruguay
    Furaha: Brazil wametinfa Fainali kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay
    Hero: Paulinho headed home the winning goal for the hosts in the 86th minute
    Shujaa: Paulinho akifunga kwa kichwa bao la ushindi dakika ya 86
    Hero: Paulinho headed home the winning goal for the hosts in the 86th minute
    Opener: Fred fired Brazil into the lead four minutes before half-time
    La kwanza: Fred akiifungia Brazil dakika nne ya kabla mapumziko
    Delight: Fred celebrates his strike in front of the adoring fans in Belo Horizonte
    Delight: Fred celebrates his strike in front of the adoring fans in Belo Horizonte
    Fred na Neymar wakishangilia mbele ya mashabiki Belo Horizonte
    Brazil 
    The crowd cheers
    Response: Edinson Cavani equalised for Uruguay early in the second half
    La kusawazisha: Edinson Cavani aliisawazishia Uruguay mapema kipindi cha pili
    Uruguay's Edinson Cavani
    Slotted: Cavani found the bottom corner as he guided the ball past the despairing Juilo Cesar
    Kudadadeeki: Cavani alivyofunga
    Slotted: Cavani found the bottom corner as he guided the ball past the despairing Juilo Cesar
    Incredible: This Brazil fanshowed his support for Hulk as his side reached the final
    Jitu Kali: Shabiki la Brazil likimsapoto Hulk
    Hulk
    Colourful: Brazil fans enjoy the atmosphere at Belo Horizonte for the semi-final
    Maua mazuri: Mashabiki wa Brazi
    Fans of Brazil
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: POULINHO AIPELEKA BRAZIL FAINALI KOMBE LA MABARA IKIIUA URUGUAY 2-1, FORLAN AKIKOSA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top