• HABARI MPYA

    Tuesday, June 25, 2013

    TENGA AWABARIKI LUNYAMILA, MATOLA KUWA MAKOCHA

    Hongera kijana; Selemani Matola akipongezwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga kwenye sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni 
    Na Mohamed Mharizo, IMEWEKWA JUNI 25, 2013 SAA 4:00 USIKU 
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, amewataka makocha kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye nchini.
    Tenga alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili leo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Kozi hiyo iliyoendeshwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), ilianza Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
    Tenga alisema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto, tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
    “Hili ndilo bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina watoto zaidi ya milioni  moja ambao wanaandaliwa, lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa katika hilo,” alisema.
    Aliwataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
    Naye Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi wa makocha kusaidia timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo nchini.
    "Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi licha ya majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii imekuwa ya mafanikio kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa zamani," alisema.
    Rahel Palangyo, mwanamke pekee kwenye kozi hiyo
    Baadhi ya washiriki waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shadrack Nsajigwa, Ibrahim Masoud, Edibily Lunyamila, Rahel Pallangyo, Ally Yusuph ‘Tigana’, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Seleman Matola na wengineo.
    Moses Mkandawile

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TENGA AWABARIKI LUNYAMILA, MATOLA KUWA MAKOCHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top