• HABARI MPYA

    Saturday, June 22, 2013

    MKENYA WANYAMA AGOMBEWA NA ARSENAL, INTER MILAN NA LIVERPOOL...SOUTHAMPTON WA KWANZA KUTOA OFA CELTIC

    IMEWEKWA JUNI 22, 2013 SAA 2:22 ASUBUHI
    KLABU ya Southampton imekubali kulipa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 kumnunua kiungo Mkenya wa Celtic, Victor Wanyama.
    Watakatifu hao, ni miongoni mwa klabu zinazoitaka saini ya Waynama – zikiwemo Arsenal, Liverpool na Inter Milan – na sasa wanaingia katika orodha ya klabu zinazogombea saini yake. 
    Wide interest: Victor Wanyama is wanted by several of Europe's biggest teams
    Mpenda kuambaa pembeni: Victor Wanyama anatakiwa na klabu kadhaa kubwa Ulaya
    High profile: The midfielder's Champions League exploits caught the eye
    Yuko juu: Kung'ara kwa kiungo katika Ligi ya Mabingwa kumemfanya amulikwe na wengi

    Kinda huyo wa umri wa miaka 21 amekuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa Celtic tangu ajiunge na klabu hiyo ya Scotland kutoka Beerschot ya Ubelgiji kwa Pauni 900,000 miaka miwili iliyopita.
    Lakini Wanyama amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake wa sasa na Celtic ambao hawatakuwa na chaguo zaidi ya kukubali faida kumuuza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MKENYA WANYAMA AGOMBEWA NA ARSENAL, INTER MILAN NA LIVERPOOL...SOUTHAMPTON WA KWANZA KUTOA OFA CELTIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top