• HABARI MPYA

    Sunday, June 23, 2013

    KARATASI YA LISTI YA KWANZA YA MAN UNITED CHINI YA SIR FERGUSON YAPIGWA MNADA PAUNI 20,000...NI MARA SITA YA BEI HALISI

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 23, 2013 SAA7:30 MCHANA 
    FOMU ya kwanza ya kabisa kikosi cha Manchester United 
    History: Sir Alex Ferguson's first Manchester United team-sheet is being auctioned
    Historia: Fomu ya kikosi cha kwanza cha Sir Alex Ferguson kuiongoza Manchester United imepigwa mnada
    alichoandika Sir Alex Ferguson akiiongoza timu hiyo kwa mara ya imeuzwa kwenye manda kwa Pauni 19,500, mara ya sita bei iliyotakiwa.
    United inajiandaa kwa maisha bila Alex Ferguson kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986, huku David Moyes akijiandaa kurithi mikoba yake kwa kuanza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
    Lakini fomu hiyo ya kikosi, iliyoandikwa kwa mkoko wa  Ferguson na kusainiwa naye katika mchezo ambao walichapwa 2-0 na Oxford United, Novemba 8, mwaka 1986 unaleta kumbukumbu ya namna gwiji huyo alivyoanza kazi.
    Iliuzwa mjini Devizes, Wiltshire, kwa Muingereza ambaye ni shabiki wa Oxford.
    Ilipangiwa kuuzwa kwa Pauni 3,000 lakini mwishowe ikafikia bei hiyo baada ya mchuano wa China na Marekani.
    Wachezaji maarufu na nyota kama Paul McGrath na Arthur Albiston wamo kwenye kikosi hicho, sambamba na wenmgine wanaokumbukwa kama kipa Chris Turner na Graeme Hogg.
    Wakati huo hakukuwa na mchezaji hata mmoja kati ya wale maarufu aliowasajili wakiwa makinda kama Peter Schmeichel au Ryan Giggs Old Trafford.
    Pia kuna kikosi cha mwisho cha Mscotland huyo ambacho kilitoka sare ya 5-5 ugenini na West Brom.
    Pia kimeandikwa kwa mkono wake Ferguson - kikionyesha nyota kadhaa wa kimataifa kama Robin Van Persie na Nahodha Michael Carrick.
    Wakongwe wa United, Ryan Giggs na Paul Scholes, ambao pia walicheza kwa mara ya mwisho, walikuwemo katika orodha ya wachezaji wa akiba.
    Pamoja na hayo, msaidizi wa David De Gea, Anders Lindegaard, jina lake lilikosewa katika karatasi hiyo kwa herufi 'r' kutumika katika jina lake.
    Final bow: Ferguson's final team-sheet against West Brom, with Anders Lindegaard's name spelt incorrectly
    Kikosi cha mwisho: Timu ya mwisho aliyoiingiza uwanjani Ferguson dhidi ya West Brom, ikionyesha jina la Anders Lindegaard limekosewa.
    Debut: Alex Ferguson (right) watches his new Manchester United side from play Oxford United's Manor Ground
    Mechi ya kwanza: Alex Ferguson (kulia) akiingalia timu yake mpya ya Manchester United katika Uwanja wa Oxford United, uitwao Manor Ground.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KARATASI YA LISTI YA KWANZA YA MAN UNITED CHINI YA SIR FERGUSON YAPIGWA MNADA PAUNI 20,000...NI MARA SITA YA BEI HALISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top