• HABARI MPYA

    Tuesday, June 25, 2013

    KAPOMBE KUWA MWAFRIKA PEKEE FC TWENTE YA UHOLANZI MSIMU UJAO, ASUBIRIWA KWA HAMU ENSCHEDE

    Kuelekea Ulaya; Shomary Kapombe
    akiwa mazoezini na Simba SC 
    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JUNI 25, 2013 SAA 4:00 ASUBUHI
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Shomary Kapombe anaweza kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee Mwafrika kwenye kikosi cha FC Twente ya Ligi Kuu ya Uholanzi msimu ujao, iwapo atapasi majaribio yake katika timu hiyo hivi karibuni. 
    FC Twente imeandika katika tovuti yake kwamba wakati wowote kuanzia sasa, Kapombe anayetumika kama beki wa kushoto siku hizi, atakuwa huko kwa majaribio. 
    Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992 aliibukia katika klabu ya Polisi Morogoro kabla ya kujiunga na Simba SC miaka mitatu iliyopita ambako anatarajiwa kumalizia Mkataba wake Desemba mwaka huu.
    Twente imejiridhisha klabu yake imekubali kumpa ruhusa kwenda kufanya majaribio nchini humo. “Tumepewa ruhusa kumuita kwa majaribio Ulaya na tunamtakia mafanikio,”imesema taarifa katika tovuti ya Twente, ambayo kwa sasa haina mchezaji Mwafrika kwenye kikosi chake cha kwanza.
    Kapombe mwenyewe ameonyesha nia thabiti ya kucheza Ulaya na amekuwa akikataa ushawishi wa timu nyingine za Tanzania zinazotaka kumng’oa Simba SC kama Yanga na Azam FC ili kusikilizia nafasi ya Ulaya.
    FC Twente maskani yake yako Enschede, ikicheza Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie na ilianzishwa mwaka 1926. Hawa ni mabingwa wa Kombe la KNVB na Johan Cruijff Schaal mwaka 2011, na wamekuwa mabingwa wa Eredivisie msimu wa 2009–2010.
    Timu hiyo, inayotumia Uwanja wa nyumbani wa De Grolsch Veste tangu 1998,  pia imeshika nafasi ya pili mara tatu Eredivisie na walikuwa pia washindi wa pili wa Kombe la UEFA msimu wa 1974–1975 na kwa ujumla wametwaa Kombe la KNVB mara tatu.

    Tanzaniaans International Shomari Kapombe op proef bij FC Twente

    Tanzaniaans International Shomari Kapombe op proef bij FC Twente

    FC Twente krijgt binnenkort waarschijnlijk de Tanzaniaan Shomari Kapombe op proef. Kapombe is een linksback die momenteel uitkomt voor Simba SC dat in eigen land één van de twee topclubs is. De melding wordt gedaan door Tanzania Soccer. Kapombe is zesvoudig international en wist één keer te scoren voor Tanzania. Hij zal ook bij andere clubs stages af gaan werken.
    Shomari Kapombe is geboren op 28 januari 1992 in Tanzania. Hij kwam enkele seizoenen gelden van de Tanzaniaanse club Police Morogoro Football Club over naar Simba SC. Hier heeft de back nog een contract tot eind december 2013.
    Zijn club Simba SC geeft de jongeling toestemming om zijn geluk te gaan beproeven in het buitenland. “We hebben groen licht gegeven om stages te gaan lopen in Europa en wensen hem heel erg veel succes. We verwachten hem na de stages wel terug om aan de voorbereiding met Simba SC deel te nemen.”
    Kapombe zelf is zeer gemotiveerd en ziet een carrière in Europa als een grote droom.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KAPOMBE KUWA MWAFRIKA PEKEE FC TWENTE YA UHOLANZI MSIMU UJAO, ASUBIRIWA KWA HAMU ENSCHEDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top