• HABARI MPYA

    Sunday, June 23, 2013

    WENGER SASA AJITOSA RASMI KUWANIA SAINI ROONEY, ATAKA KUMTUMIA KAMA KIUNGO MSHAMBULIAJI NYUMA YA HIGUAIN

    IMEWEKWA JUNI 23, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
    KLABU ya Arsenal baada ya kumalizana kwa dau la Pauni Milioni 22 na Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid, sasa inahamishia nguvu zake kwa mshambuliaji wa Manchester United, anayeuzwa Pauni Milioni 20, Wayne Rooney - huku kocha Arsene Wenger akiwa amedhamiria kuendelea kumtumia katika nafasi ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Muargentina huyo.
    Higuain ni mchezaji ambaye Arsenal sasa wana uhakika wa kumnasa, huku Carlo Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao wa Hispania, akitarajiwa kutua leo kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.
    Highly rated: But Wayne Rooney's future remains uncertain
    Matawi ya juu: Lakini mustakabali wa Wayne Rooney bado haueleweki
    Man United's Wayne Rooney
    Lakini katika uhamisho huo wa Rooney, Arsenal italazimika kumlipa mshahara wake wa Pauni 220,000 kwa wiki, ambao ni mkubwa mno kulingana na tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu 'bakhili'.
    Wenger haoni kama Rooney ni mshambuliaji wa kati, lakini kama kiunganishi, baina ya kiungo na Higuain — nafasi ambayo mchezaji mwenyewe amesema inamfaa. 
    Lakini Chelsea pia inamtaka Rooney na kocha mpya wa United, David Moyes anatarajiwa kukutana na Rooney wiki mbili zijazo, hivyo uwezekano wa yeye kujiunga na klabu hiyo ya London bado mdogo.
    United haitataka kumuuza Rooney kwa Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa washindani wao wakuu katika mbio za ubingwa na matumaini ya mchezaji huyo yanabakia katika kikao chake na Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo mpya mzuri Old Trafford, hususan baada ya klabu kusema hajawahi kuomba kuondoka United.
    Hilo ni suala lililotokana na wasiwasi wa Rooney juu ya uhusiano wake na mashabiki wa United. Rooney anatarajia kikao kama alichowahi kufanya na kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita, cha binafasi kujadili mustakabali wake katika klabu.
    Arsenal imetenga bajeti ya kutosha kupambana katoka soko la usajili, lakini tatizo ni kwamba wataweza kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa sababu ni wenye kiu ya mataji, vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo vimekuwa adimu.
    Ambitious: Arsenal's Arsene Wenger is ready to join the race for Rooney
    Mzee wa matarajio: Arsene Wenger wa Arsenal yuko tayari kugombea saini ya Rooney.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WENGER SASA AJITOSA RASMI KUWANIA SAINI ROONEY, ATAKA KUMTUMIA KAMA KIUNGO MSHAMBULIAJI NYUMA YA HIGUAIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top