• HABARI MPYA

    Friday, June 21, 2013

    TORRES APIGA NNE PAMOJA NA KUKOSA PENALTI HISPANIA IKIIFUMUA 10-0 TAHITI

    IMEWEKWA JUNI 21, 2013 SAA 7:00 USIKU
    MSHAMBULIAJI Fernando Torres amefunga mabao manne pamoja na kukosa penalti wakati Hispania ikiifumua 10-0 Tahiti katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mabara.
    Alifunga mabao hayo katika dakika za tano, 33, 57 na 78 wakati David Villa alipiga Hat-trick katika dakika za 39,49 na 64, David Silva akafunga mawili dakika za 31 na 89 na Juan Mata pia akafunga dakika ya 66 kuiwezesha Hispania kupaa kileleni mwa Kundi B mbele ya Nigeria, ambao muda huu wanamenyana na Uruguay.
    Kikosi cha Hispania kilikuwa: Reina, Albiol, Azpilicueta, Ramos/Navas dk46, Monreal, Martinez, Cazorla/Iniesta dk76, Silva, Villa, Torres na Mata/Fabregas dk69.
    Tahiti: Roche, Ludivion, Vallar, Lemaire/Vero dk73, Aitamai, J Tehau, A Tehau/T Tehau dk53, Vahirua, Caroine, Bourebare/L Tehau dk69 na Chong Hue.
    Here we go: Fernando Torres was on fire for Spain against Tahiti as the world champions eased to a win
    Tunapaa: Fernando Torres alikuwa moto usiku huu
    Me too: Barcelona striker David Villa also showed no mercy to the part-timers
    Nami pia: Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa alifunga pia
    Caught out: Torres slid the ball in at the near post to put Spain in the lead early in the match
    Torres akifunga

    KUNDI B KOMBE LA MABARA

    TimuMechiKushindaSareKufungwaMabao ya kufungaMabao ya kufungwaPointi
    Spain22001216
    Nigeria1100613
    Uruguay1001120
    Tahiti20021160

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TORRES APIGA NNE PAMOJA NA KUKOSA PENALTI HISPANIA IKIIFUMUA 10-0 TAHITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top