• HABARI MPYA

    Thursday, June 20, 2013

    LIVERPOOL YASAJILI KIFAA CHA BARCELONA KUZIBA PENGO LA SUAREZ

    IMEWEKWA JUNI 20, 2013 SAA 4:00 USIKU
    MSHAMBULIAJI wa Sevilla, Luis Alberto atafanyiwa vipimo vya afya Liverpool kesho baada ya klabu hizo mbili kufikia makubaliano ya kuuziana nyota huyo kwa Pauni Milioni 6.8.
    Kinda huyo wa umri wa miaka 20, ambaye atasaini Mkataba wa miaka minne, amekuwa akicheza kwa mkopo Barcelona B na alitarajiwa kubaki Sevilla, lakini kwa fedha iliyotolewa klabu hiyo imeamua kumuacha aondoke.
    Barcelona imeamua kuachana na nia ya kumsajili moja kwa moja baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo, na Alberto atakuwa mshambuliaji wa pili kusajiliwa Liverpool baada ya Iago Aspas kutoka Celta Vigo.
    New man: Alberto is on his way to Anfield after cash-strapped Sevilla accepted a £6.8m deal
    Mtu mpya: Alberto yuko njiani kutua Anfield kutoka Sevilla kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 6.8

    Usajili huu unaleta shaka juu ya mustakabali wa mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez, ambaye amekuwa akihusishwa na kuondoka majira haya ya joto.

    REKODI YA LUIS ALBERTO NGAZI YA KLABU:

    2009-2012 - Sevilla B Mechi 77 mabao 25
    2011 - hadi sasa - Sevilla Mechi 7 hakufunga bao
    2012-13 - Barcelona B (mkopo) Mechi 37 mabao 11
    Habari hizo zinakuja siku moja baada ya Mkurugenzi wa Michezo wa Sevilla, Monchi kusema ofa iliyotolewa na Liverpool ni kiduchu kwa Alberto - lakini klabu hiyo ya Merseysiders imekamilisha mpango.
    Alberto ameichezea mara moja timu ya taifa ya vijana ya Hispania chini ya umri wa miaka 21, na amefunga mabao 11 katika mechi 38 alizoichezea Barcelona B msimu uliopita.
    Amefunga mabao 25 katika mechi 77 alizoichezea Sevilla B kati ya mwaka 2009 na 2012, na ameichezea klabu hiyo mechi saba za La Liga.
    Replacement? The deal could be an indicator that Luis Suarez is on his way out of the Anfield club
    Mbadala wake? Usajili huu ni dalili kwamba anatafutwa mbadala wa Luis Suarez anayetaka kuondoka Anfield 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIVERPOOL YASAJILI KIFAA CHA BARCELONA KUZIBA PENGO LA SUAREZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top