WABABE wa Yanga SC katika michuano ya Afrika, Etoile du Sahel wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Etoile iliyitoa Yanga SC kwa jumla ya mabao 2-1 ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kushinda 1-0 nyumbani, usiku huu imeitoa Raja Casablanca ya Morocco kwa kuifunga mabao 3-0 mjini Sousse hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 2-0 Morocco.
Hii ilikuwa ni hatua ya mchujo kuwania kupangwa katika makundi, iliyozikutanisha timu zilizosonga mbele Kombe la Shirikisho dhidi ya zilizotolewa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Etoile du Sahel waliitoa Yanga SC 'kwa mbinde' katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho.
AS Vita ya DRC imeshindwa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya ushindi wa maabo 3-2 jioni ya leo dhidi ya Stade Malien Uwanja wa Raphael Tata mjini Kinshasa.
Malien imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3 baada ya awali kushinda 2-0 mjini Bamako.
'Les Blancs' wanaungana na Esperance katika Kundi A.
katika mechi nyingine za leo, CS Sfaxien imetinga pia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas baada ya sare ya 1-1 jioni ya ikitoka kushinda 2-0 mchezo wa kwanza nyumbani.
Zamalek imeifunga 3-1 Sanga Balende na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 1-0, Al Ahly imesonga mbele kwa penalti 5-4 dhidi ya Club Africain baada ya sare ya jumla ya 3-3 kila timu ikishinda 2-1 nyumbani kwake.
Katika mechi za jana, AC Leopards ya Kongo ilitinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa mabao 3-1 leo na Warri Wolves ya Nigeria.
Lakini ushindi wa kwanza nyumbani wa mabao 3-0 mjini Dolisie umewasaidia Wakongo hao licha ya kipigo cha leo Uwanja wa Warri City.
Hearts of Oak ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Esperance hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-1, baada ya awali kufungwa 4-0 Tunsia.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini iliifunga 4-1 AS Kaloum na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya awali kufungwa 2-0 mjini Bamako.
Etoile iliyitoa Yanga SC kwa jumla ya mabao 2-1 ikitoa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kushinda 1-0 nyumbani, usiku huu imeitoa Raja Casablanca ya Morocco kwa kuifunga mabao 3-0 mjini Sousse hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 2-0 Morocco.
Hii ilikuwa ni hatua ya mchujo kuwania kupangwa katika makundi, iliyozikutanisha timu zilizosonga mbele Kombe la Shirikisho dhidi ya zilizotolewa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Etoile du Sahel waliitoa Yanga SC 'kwa mbinde' katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho.
AS Vita ya DRC imeshindwa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya ushindi wa maabo 3-2 jioni ya leo dhidi ya Stade Malien Uwanja wa Raphael Tata mjini Kinshasa.
![]() |
| Etoile du Sahel waliitoa Yanga SC katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika na sasa wametinga hatua ya makundi |
ZILIZOTINGA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO
Stade Malien (Mali), CS Sfaxien (Tunisia), Etoile du Sahel- (Tunisia), Zamalek (Misri), Al Ahly (Misri), AC Leopards (Kongo), Esperance (Tunisia) na Orlando Pirates (Afrika Kusini)
|
'Les Blancs' wanaungana na Esperance katika Kundi A.
katika mechi nyingine za leo, CS Sfaxien imetinga pia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas baada ya sare ya 1-1 jioni ya ikitoka kushinda 2-0 mchezo wa kwanza nyumbani.
Zamalek imeifunga 3-1 Sanga Balende na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 1-0, Al Ahly imesonga mbele kwa penalti 5-4 dhidi ya Club Africain baada ya sare ya jumla ya 3-3 kila timu ikishinda 2-1 nyumbani kwake.
Katika mechi za jana, AC Leopards ya Kongo ilitinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa mabao 3-1 leo na Warri Wolves ya Nigeria.
Lakini ushindi wa kwanza nyumbani wa mabao 3-0 mjini Dolisie umewasaidia Wakongo hao licha ya kipigo cha leo Uwanja wa Warri City.
Hearts of Oak ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Esperance hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-1, baada ya awali kufungwa 4-0 Tunsia.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini iliifunga 4-1 AS Kaloum na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya awali kufungwa 2-0 mjini Bamako.

.png)
0 comments:
Post a Comment