Na Mwandishi Wetu, BULAWAYO
MSAFARA wa Yanga SC umewasili salama mjini Bulawayo majira ya Saa 1 na ushei usiku ukitokea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano, hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, FC Platinum.
Hiyo inafuatia msafara huo kuchelewa kuodoka Dar es Salaam baada ya kugandishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tangu saa 4 asubuhi hadi saa 7 na ushei mchana kwa madai uongozi wa klabu hiyo ulikuwa haujalipia ndege.
Yanga SC imekodi ndege ya Serikali kwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, FC Platinum.
Hata hivyo, ilidaiwa uongozi wa ndege uligoma kuwapakia wachezaji hao hadi malipo yafanyike- na sakata hilo likatatuliwa saa 7 na ushei mchana na wachezaji wakapanda ndege kuondoka.
Kutokana na kuchelewa kufika, Yanga SC wameshindwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja Mandava ambao watautumia kwa mchezo huo kesho.
Maana yake Yanga SC itaujaribu Uwanja huo kesho muda mfupi kabla ya mchezo wakati wa kufanya mazoezi ya kuipasha miili ya wachezaji joto.
Kikosi cha wachezaji 18 wa Yanga SC kimekwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Platinum wanatakiwa kushinda mabao 4-0 Uwanja wa Mandava kesho ili kwenda 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, baada ya awali timu hiyo yenye maskani yake Zvishavane kufungwa mabao 5-1 Dar es Salaam.
Wachezaji walioondoka ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
Viungo ni Salum Telela, Said Juma, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na washambuliaji Danny Mrwanda, Amisi Tambwe na Hussein Javu.
Benchi la Ufundi litaongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Sufiani Juma, mtunza vifaa, Mahmoud Omar ‘Mpogolo’ na Mchua misuli Jacob Onyango.

![]() |
| Baadhi ya wachezaji wa Yanga SC walio safarini Bulawayo kutoka kulia kipa Deo Munishi 'Dida', Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Mbuyu Twite na Juma Abdul. |
Hata hivyo, ilidaiwa uongozi wa ndege uligoma kuwapakia wachezaji hao hadi malipo yafanyike- na sakata hilo likatatuliwa saa 7 na ushei mchana na wachezaji wakapanda ndege kuondoka.
Kutokana na kuchelewa kufika, Yanga SC wameshindwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja Mandava ambao watautumia kwa mchezo huo kesho.
Maana yake Yanga SC itaujaribu Uwanja huo kesho muda mfupi kabla ya mchezo wakati wa kufanya mazoezi ya kuipasha miili ya wachezaji joto.
Kikosi cha wachezaji 18 wa Yanga SC kimekwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Platinum wanatakiwa kushinda mabao 4-0 Uwanja wa Mandava kesho ili kwenda 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, baada ya awali timu hiyo yenye maskani yake Zvishavane kufungwa mabao 5-1 Dar es Salaam.
Wachezaji walioondoka ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
Viungo ni Salum Telela, Said Juma, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na washambuliaji Danny Mrwanda, Amisi Tambwe na Hussein Javu.
Benchi la Ufundi litaongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Sufiani Juma, mtunza vifaa, Mahmoud Omar ‘Mpogolo’ na Mchua misuli Jacob Onyango.

.png)
0 comments:
Post a Comment