• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    STAND UNITED NA JKT RUVU KAMBARAGE, JUMAMOSI AZAM NA KAGERA CHAMAZI, MBEYA CITY NA SIMBA SOKOINE

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho siku ya ijumaa kwa mchezo mmoja, wenyeji timu ya Stand United watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea kutimua vumbi siku ya jumamosi  kwa michezo mitatu, mjini Morogoro wenyeji Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
    Jijini Mbeya wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Azam Complex.
    Makocha wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic (kushoto) na Msaidizi wake, Suleiman Matola kulia 

    Jumapili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea  kwa maafande wa timu ya Ruvu Shooting  kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mabatini - Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED NA JKT RUVU KAMBARAGE, JUMAMOSI AZAM NA KAGERA CHAMAZI, MBEYA CITY NA SIMBA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top