• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2015

    MAALBINO WAWALIZA WACHEZAJI SIMBA SC SHINYANGA

    Na Philip Chimi, SHINYANGA
    WAKATI jioni ya leo inacheza na Kagera Sugar mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, SImba SC imefanya ziara fupi katika kituo cha kulea watu wenye ulemavu ngozi, maarufu kama Albino kilichopo Buhangija mjini Shinyanga.
    Wachezaji wote na viongozi waliongozana na timu Shinyanga kwa ajili ya mechi hiyo leo walifika katika kituo hicho kuwafariji ndugu zao hao. 
    Akisoma risala fupi iliyo andaliwa na wachezaji wa timu, kiungo wa Simba SC Ibrahim Twaha ‘Messi’ amesama wao kama wachezaji wa klabu hiyo wameguswa mno na mauaji ya ndugu zao Albino. “Na kwa kuwa sisi ni timu kubwa hapa nchini, tumeona ni vyema kuja kuwapa nguvu na kuwatia moyo watoto, ambao wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao,:”amesema Twaha.
    Kiungo wa Simba SC, Ibrahim Twaha 'Messi' alijikuta anamwaga machozi kwa hisia kutokana na mateso wanayopata Maalbino
    Nyota wa Simba SC, Emmanuel Okwi akiwa amepakata watoto wenye ulemavu wa ngozi leo
    Mkuu Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara alikuwa mwenye simanzi kituoni hapo

    Ameongeza kwamba wachezaji wote na wa Simba  kwa ujumla watakuwa mabalozi wa kupinga vikali vitendo hivyo vya ukatili na hivyo kuwasihi wachezaji wenzake kuwa mstari wa mbele kupinga na kuwalinda wale wote wenye ulemavu wa ngozi nchini.
    Hata hivyo, Twaha alishindwa kumalizia risara hiyo baada ya kutokwa machozi kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya matatizo wanayopata Maalbino, hali iliyomfanya Kocha Mkuu, Mserbia Goran Kuponovic na wachezaji wote wa Simba kuangua kilio mbele ya watoto na walio wa kituo hicho.
    Naye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano  wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kwamba Simba SC imekuwa klabu ya kwanza kufika katika kituo hicho.
    Simba SC pia walikabidhi zawadi zmbalimbali kituoni hapo, ikiwemo vinywaji kama soda na maji, fedha tasilim Shi. Miioni 1 a pia wametoa nafasi ya watoto 50 leo kwenda kuona mchezo wao dhidi ya Kagera.
    Jumla ya watoto waliopo kituoni hapo ni 374 kati yao watoto 270 ni wenye ulemavu wa ngozi 40, wasioona na 64 ni viziwi .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAALBINO WAWALIZA WACHEZAJI SIMBA SC SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top