KUNDI la Friends Of Simba (F.O.S) limeahidi kutoa rambirambi ya Sh. Milioni 2 kwa familia za wapenzi wa klabu ya Simba waliofariki ajalini jana wakiwa njiani kuelekea Shinyanga kuishagilia timu hiyo ikimenyana na Kagera Sugar leo.
Watu sita wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 15 kujeruhiwa vibaya baada ya ajali ya basi dogo aina ya Coaster eneo la Mvomero, Morogoro jana wakiwa njiani kuelekea Shinyanga kuishangilia timu yao.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa wana Simba wenzao hao, tena wakiwa njiani kwenda kuishangilia timu.
![]() |
| Zacharia Hans Poppe ametoa salamu za rambirambi kwa msiba wa Simba Ukawa |
Poppe anasema kwamba ingawa gari walilokuwa wanatumia lilikuwa limeandikwa Simba Ukawa ambao ni wapinzani wa uongozi uliopo madarakani chini ya Rais Evans Aveva, lakini anachojua ni Simba wenzao tu.
“Ni pigo kubwa kwa kweli kupoteza watu hao, ambao tena walikuwa wanakwenda kuisapoti timu. Kwa kweli tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na tunaungana na wana Simba wote, kuomboleza msiba huu,”amesema Poppe.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba tayari baadhi ya memba wa F.O.S. wameanza kufuatilia taarifa za msiba ili kuweza kushiriki kikamilifu.
![]() |
| Gari lililopata ajali baada ya kuinuliwa |




.png)
0 comments:
Post a Comment