• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    KWA REKODI HII, YANGA IPO TAYARI KUWANG’OA WAARABU AFRIKA?

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    CHINI ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm, Yanga SC mwaka jana ilivunja mwiko wa kutozifunga timu za Kaskazini mwa Afrika, baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri.
    Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwa mara ya kwanza, Yanga SC ikashangilia ushindi dhidi ya Ahly, timu ya Misri na Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla.
    Hata hivyo, katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza mjini Alexandrie, Misri, wenyeji Ahly walilipa kisasi kwa ushindi wa 1-0, hivyo mchezo ukahamia kwenye dakika za nyongeza na baadaye penalti, ambako ilitolewa kwa penalti 4-3.
    Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto alifunga bao pekee Yanga ikiilaza 1-0 Al Ahly mwaka jana

    Wakiwa katika michuano tofauti na ya mwaka jana, Yanga SC watakutana na mpinzani tofauti pia kutoka Kaskazini mwa Afrika mwishoni mwa wiki hii.
    Yanga SC wanaikaribisha Etoile du Sahel ya Tunisia Jumamosi katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika. 
    Tayari Yanga SC imekwishavunja mwiko wa kutozifunga timu za Kaskazini mwa Afrika na Jumamosi itajaribu kuendelea kuzifunga japo katika Uwanja wa nyumbani.
    Lakini wiki mbili baadaye, Yanga SC itakuwa inawania kujiwekea rekodi mpya, kuitoa kwenye mashindano timu ya Kaskazini mwa Afrika.  
    Waswahili wanasema hakuna kisichowezekana chini ya jua, lakini Yanga SC ipo tayari kwa hilo?
    Makocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm kulia na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa wanamtegemea sana Mrisho Ngassa katika kampeni ya kuwatoa Etoile du Sahel Kombe la Shirikisho

    REKODI YA YANGA DHIDI YA TIMU ZA KASKAZINI 
    Ligi ya Mabingwa Afrika; 1982
    RAUNDI YA PILI:
    Al- Ahly 5-0 Yanga (Misri) 
    Yanga SC 1-1 Al- Ahly (Dar) 

    Ligi ya Mabingwa; 1988
    RAUNDI YA KWANZA:
    Yanga 0-0 Al-Ahly (Dar)
    Al- Ahly 4-0 Yanga (Misri) 

    Ligi ya Mabingwa; 1992
    RAUNDI YA KWANZA:
    Yanga 0-2 Ismailia (Dar)
    Ismailia 1-1 Yanga (Misri)

    Ligi ya Mabingwa; 1998
    MECHI ZA KUNDI B:
    Raja Casablanca 6-0 Yanga (Morocco) 
    Yanga Vs Raja Casablanca 3-3 (Dar) 

    Ligi ya Mabingwa; 2007:
    RAUNDI YA PILI: 
    Esperance 3-0 Yanga (Tunisia)
    Yanga SC 0-0 Esperance (Dar) 
    (Yanga iliingia kwenye kapu la kuwania kucheza Kombe la Shirikisho na kutolewa na El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 2-0) 

    Ligi ya Mabingwa; 2009
    RAUNDI YA KWANZA
    Al Ahly 3-0 Yanga (Misri)
    Yanga 0-1 Al Ahly (Dar)

    Ligi ya Mabingwa; 2012
    RAUNDI YA KWANZA
    Yanga 1-1 Zamalek (Dar)
    Zamalek 1-0 Yanga (Misri)

    Ligi ya Mabingwa; 2014
    RAUNDI YA KWANZA
    Yanga SC 1-0 Al Ahly (Dar)
    Al Ahly 1-0 Yanga SC (Misri)
    (Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)

    Kombe la Washindi; 2000
    RAUNDI YA KWANZA
    Yanga 1-1 Zamalek (Dar)
    Zamalek 4-0 Yanga SC (Misri)

    Kombe la Shirikisho; 2008
    RAUNDI YA KWANZA; 
    Al-Akhdar 1-0 Yanga (Libya) 
    Yanga SC 1-1 Al-Akhdar (Dar)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KWA REKODI HII, YANGA IPO TAYARI KUWANG’OA WAARABU AFRIKA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top