• HABARI MPYA

    Thursday, April 16, 2015

    KIINGILIO YANGA NA ETOILE ELFU TANO KWA ‘WAGUMU’, KULE KWA ‘WASHUA’ 40,000

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika baina 
    Yanga SC na Etoile du Sahel ya Tunisia Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa ni Sh. 5,000.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kiingilio hicho kitahusu majukwaa yenye viti vya rangi ya bluu na kijani.
    Muro amesema viingilio vingine vitakuwa ni Sh. 10,000 kwa viti ya Rangi ya Chungwa, Sh. 20,000 VIP C, Sh. 30,000 VIP B na Sh. 40,000 VIP A.
    Ametaja maeneo ya mauzo ya tiketi kuwa ni Uwanja wa Karume, Billicanas, Feri, Dar Live, Buguruni Sheli, Ubungo Stendi ya mabasi, Uwanja w Taifa, makao makuu ya Yanga makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na Mwembe Yanga, Tandika. 
    Marefa watakaochezesha mechi hiyo kutoka  Msumbiji, Samuel Chirindza atakayesaidiwa na Arsenio Chadreque Marengula, Celio de Jesus Mugabe washika vibendera, Jose Maria Rachide mwamuzi wa akiba mezani na Kamisaa Salah Ahmed Mohamed Saleh kutoka Sudan wanatarajiwa kuwasili kesho asubuhi.
    Wakati Yanga SC imeweka kambi hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam huku ikiendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa, 
    Etoile du Sahel wao wanatarajiwa kuwasili ‘usiku wa manane’ leo kuelekea Alfajiri ya kesho kwa ndege maalum wakiwa na msafara wa watu 55.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIINGILIO YANGA NA ETOILE ELFU TANO KWA ‘WAGUMU’, KULE KWA ‘WASHUA’ 40,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top