Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MAREFA watakaochezesha mechi mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baina wenyeji Yanga SC na Etoile du Sahel ya Tunisia Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wanatarajiwa kuwasili kuwasili kesho asubuhi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, marefa hao kutokaa Msumbiji, Samuel Chirindza atakayesaidiwa na Arsenio Chadreque Marengula, Celio de Jesus Mugabe washika vibendera na Jose Maria Rachide atakuwa mwamuzi wa akiba mezani wamethibitisha kuwasili kesho.
Muro amesema Kamisaa ni Salah Ahmed Mohamed Saleh kutoka Sudan, pia atawasili kesho.
Muro amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri na kikosi chao kipo kambini hoteli ya Tansoma, eneo la Gerezani, Dar es Salaam huku kikiendelea na mazoei Uwanja wa Taifa
Etoile du Sahel wao wanatarajiwa kuwasili ‘usiku wa manane’ leo kuelekea Alfajiri ya kesho kwa ndege maalum, tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi na Muro amesema wanakuja na msafara wa watu 55.
Na ESS watapanda ndege moja na ndugu zao, Esperance ya Tunis kwenda kwenye mechi za awali za michuano ya Afrika hatua hii. Esperance wanakwenda kucheza na El Marreikh nchini Sudan.
Safari itaanza Alhamisi, yaani kesho na ndege itawateremsha kwanza Esperance nchini Sudan kabla ya kuja Dar es Salaam.
Na wakati wa kurudi pia, ndege itawapitia Esperance nchini Sudan ambao wanacheza El Merreikh Jumamosi pia.
Mechi kati ya Yanga SC dhidi ya Etoile itakayoanza Saa 9:00 Alasiri.

.png)
0 comments:
Post a Comment