Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Coastal Union leo jioni wanacheza na wenyeji wao, Fanja SC kwenye Uwanja wa Seeb mjini Muscat, Oman katika mchezo wa kirafiki.
Huo utakuwa mchezo wa tatu katika ziara ya timu hiyo ya mkoa wa Tanga nchini Oman, baada ya awali kushinda mechi mbili, kwanza 2-0 dhidi ya Musannaa na baadaye 2-0 pia dhidi ya Nadi Oman.
Lakini mchezo wa leo jioni unatarajiwa kuwa mgumu kidogo kwa Coastal, kwa sababu inacheza na washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Oman msimu uliopita na timu tishio zaidi kuliko wapinzani wake wa awali.
Coastal Union imefikia katika hoteli ya Taj karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Muscat na imekuwa ikijifua vikali katika kambi yake ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.
Kocha Mkenya wa Coastal, Yussuf Chipo amekuwa akitumia wachezaji wengi waliopandishwa kutoka timu ya vijana katika ziara ya hapa, lakini kwa uzito wa mechi ya leo, anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake.
Kwa sasa kikosi cha Fanja chini ya kocha wake, Mtunisia, Hicham Jadran Ghazouani kina mchezaji mmoja tu wa kigeni, mshambuliaji Ely Cisse kutoka Senegal.
Fanja ilipoteza makali yake miaka ya 1990 mwishoni hadi 2000 mwanzoni baada ya kuyumba kiuchumi, kabla ya mwaka 2006, bilionea Hamyar bin Nasser Ismaili kurejea kuinusuru na sasa imekuwa tishio tena.

![]() |
| Fanja ya sasa si ya kuchezea, ni tishio |

.png)
0 comments:
Post a Comment