• HABARI MPYA

    Wednesday, November 06, 2013

    SIMBA SC NA ASHANTI LEO TAIFA...ILIKUWA BURUDANI YA SOKA NA KUNG'FU

    Mshambuliaji wa Simba SC, Mrundi Amisi Tambwe akiwatoka mabeki wa Ashanti United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 4-2.


    Beki wa Ashanti akimpiga teke la kung'fu beki wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya'


    Beki mcheza rafu wa Ashanti akimpa kitu Amisi Tambwe wa Simba SC


    Ramadhani Singano 'Messi' akimgeuza beki wa Ashanti


    Beki wa Ashanti akiupitia mpira miguuni mwa Tambwe 


    Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe akimtibu Amisi Tambwe


    Yalaa! Tambwe akiugulia maumivu baada ya kuchezewa rafu na beki wa Ashanti


    Wauaji watatu; Kutoka kulia Ramadhani Singano 'Messi', Betram Mombeki na Amisi Tambwe wakishangilia bao la nne


    Messi akiwatoka mabeki wa Ashanti 


    Betram Mombeki akimtoka beki wa Ashanti


    Said Ndemla akimpiga changa mbaya mchezaji wa Ashanti


    Beki Haruna Shamte wa Simba SC akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Ashanti


    Betram Mombeki akienda chini baada ya kupitiwa na mpira wake na beki wa Ashanti


    Beki wa Ashanti akienda chini baada ya kupamiwa na Amisi Tambwe kushoto


    Jonas Mkude amemlamba chenga Paul Maona wa Ashanti


    Simba SC wakishangilia moja ya mabao yao


    Ashanti United wakishangilia bao lao la kwanza


    11 wa Simba SC walioanza leo


    11 wa Ashanti walioanza leo


    Sijui nihame hii timu; Shabiki wa kike wa Ashanti kulia akiwa mwenye majonzi baada ya timu yake kufungwa bao la nne


    Nifukuze makocha wakati tumeshinda nne; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (kushoto) akizungumza na Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Kinesi' na mwanachama wa timu hiyo, Crescentius John Magori kulia baada ya mechi

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC NA ASHANTI LEO TAIFA...ILIKUWA BURUDANI YA SOKA NA KUNG'FU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top