• HABARI MPYA

    Saturday, November 30, 2013

    ZANZIBAR YAWANIA ROBO FAINALI LEO, KENYA YAJARIBU BAHATI KWA SUDAN KUSINI NYAYO

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    ZANZIBAR leo inatarajiwa kucheza mechi yake ya pili ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kwa kumenyana na Ethiopia, Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
    Zanzibar Heroes ambayo iliifunga Sudan Kusini 2-1 katika mchezo wa kwanza, iwapo itafanikiwa kushinda leo itakuwa imejihakikishia kuingia Robo Fainali za michuano hiyo.
    Lakini pia itaendelea kubaki katika mazingira mazuri kwa matokeo yoyote yale, iwapo tu Kenya itaifunga Sudan katika mchezo wa pili jioni ya leo kwenye Uwanja huo huo.
     
    Tayari kiungo tegemeo wa Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe’ amesema kwamba wamewaona wapinzani wao wengine katika Kundi hilo, Kenya na Ethiopia na pamoja na kuwasifu ni wazuri, lakini amesema hawawatishi hata kidogo. 
    “Sisi baada ya mechi yetu (na Sudan Kusini) tulipanda jukwaani kutazama mechi ya Kenya na Ethiopia kwa kuwa hao ndiyo wapinzani wetu wajao. Kwa kweli niseme tu timu zote nzuri, lakini sisi hazitutishi, tutapambana nazo ili tuzifunge na kuingia Robo Fainali,”alisema kiungo huyo wa Coastal Union ya Tanga.
    Selembe alisema wangeweza kushinda mabao mengi dhidi ya Sudan Kusini kama si kupoteza nafasi nyingi walizotengeneza.
    “Na pia ilionekana wakati fulani kama tumezidiwa ni kwa sababu tu ya uchovu wa safari na hali ya hewa ya huku (baridi), lakini tunatarajia kuanzia mchezo ujao tutacheza ile soka yetu haswa ambayo watu wanaifahamu,”alisema. 
    Zanzibar itakamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Kenya Desemba 3.  

    MISIMAMO YA MAKUNDI CHALLENGE 2013

    Kundi A
    P W D L GF GA GD Pts
    Zanzibar 1 1 0 0 2 1 1 3
    Ethiopia 1 0 1 0 0 0 0 1
    Kenya 1 0 1 0 0 0 0 1
    Sudan K 1 0 0 1 1 2 -1 0

    Kundi B
    P W D L GF GA GD Pts
    Burundi 1 1 0 0 2 0 0 3
    Tanzania 1 0 1 0 1 1 0 1
    Zambia 1 0 1 0 1 1 0 1
    Somalia 1 0 0 1 2 0 -2 0

    Kundi C
    P W D L GF GA GD Pts
    Sudan 1 1 0 0 3 0 3 3
    Uganda 1 1 0 0 1 0 1 3
    Rwanda 1 0 0 1 0 1 -1 0
    Eritrea 1 0 0 1 3 0 -3 0

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR YAWANIA ROBO FAINALI LEO, KENYA YAJARIBU BAHATI KWA SUDAN KUSINI NYAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top