• HABARI MPYA

    Thursday, November 07, 2013

    ARSENAL YAIKALISHA BORUSSIA DORTMUND, ETO'O APIGA MBILI CHELSEA IKIUA WAJERUMANI...MESSI KAMA KAWA, AIPIGIA MBILI BARCA IKIINYANYASA AC MILAN ULAYA

    BAO pekee la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund nchini Ujerumani.
    Hilo linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika michuano ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza vyema usiku huu na kabla ya Arsenal kupata bao lake, hawakuweza kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga.
    Borussia ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa, iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart katika ligi ya kwao, Bundesliga, lakini ilikalishwa na mtutu mmoja wa bunduki. 
    Dortmund; Weidenfeller 6, Grosskreutz 7, Papastathopoulos 6, Subotic 7, Schmelzer 6, Sahin 5, Bender 5 (Hofmann 75, 5), Blaszczykowski 6 (Aubameyang 74, 5), Mkhitaryan 6, Reus 6 (Schieber 86), Lewandowski 6. 
    Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta, Cazorla/Monreal dk75, Ozil, Rosicky/Vermaelen dk91 na Giroud/Bendtner dk90.

    Zama za ushindi: Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao pekee la ushindi la ArsnalBravery: Ramsey sticks his head where it hurts to guide home the winner
    Ramsey akifunga bao muhimuBravery: Ramsey sticks his head where it hurts to guide home the winner
    Sucker-punch: Dortmund had had the best of the chances up to that point
    Dortmund ilipata nafasi nyingi nzuri ikapotezaSucker-punch: Dortmund had had the best of the chances up to that point
    groupf.PNG

    MECHI ZILIZOBAKI ZA ARSENAL:

    Marseille (H), Novemba 27
    Napoli (A), Desemba 11
    Katika mechi nyingine, Barcelona imeifunga AC Milan mabao 3-1 Uwanja wa Camp Nou, Lionel Messi akifunga mawili dakika ya 30 na 83, wakati lingine limefungwa na Busquets dakika ya 40, huku Pique akijifunga dakika ya 45 kuwapatia wageni bao la kufutia machozi.
    Barcelona: Valdes; Dani Alves, Pique, Mascherano, Adriano; Xavi/Song dk88, Busquets, Iniesta/Fabregas dk78, Alexis, Messi na Neymar/Pedro dk85)
    AC Milan: Abbiati; Abate, Zapata, Mexes, Emanuelson; Muntari, Montolivo, De Jong, Poli/Birsa dk74', Kaka/Matri dk84, Robinho/Balotelli dk46.
    High five! Barcelona's Lionel Messi (left) celebrates the final goal with provider Cesc Fabregas
    Tano juu! Nyota wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akishangilia bao lake la mwisho na mpishi wake, Cesc Fabregas
    Back of the net! Messi seals victory with his second goal after an intricate passing move
    Kitu nyavuni! Messi akifunga bao la pili

    Nayo Chelsea imeifumua 3-0 Schalke 04, mabao ya Samuel Eto'o dakika ya 31 na 54 na Demba Ba dakika ya 83.
    Chelsea: Cech, Ivanovic, Azpilicueta, Mikel, Cahill, Terry, Willian, Ramires, Eto'o/Ba dk77, Oscar/Lampard dk81 na Schürrle/De Bruyne dk78.
    Schalke: Hildebrand, Uchida, Aogo, Neustädter, Höwedes, Matip, Draxler/Clemens dk62,  Jones, Szalai, Boateng/Kolasinac dk77 na Fuchs/Meyer dk67.
    Too quick: Samuel Eto'o blocks Timo Hildebrand's attempted clearance to give Chelsea the lead
    Haraka mno: Samuel Eto'o aliuzuia mpira wa Timo Hildebrand kabla ya kuifungia Chelsea baola kwanzaClosing down: Eto'o chases towards Schalke goalkeeper Timo Hildebrand
    Eto'o akimfuata kipa wa Schalke, Timo HildebrandBlocked: Eto'o gets in the way of Hildebrand's kick as he attempts to clear the ball
    Anauzuia: Eto'o aliunasa mpira na kuusukumia nyavuniGoing in: Eto's block sends the ball flying into the back of the Schalke net to give Chelsea the lead
    Eto's alifunga bao tamu sanaMutual appreciation: Eto'o celebrates with manager Jose Mourinho after giving Chelsea the lead
    Eto'o akishangilia na kocha Jose Mourinho Cool finish: Eto'o grabs his second goal of the night by neatly slotting the ball past Hildebrand
    Eto'o akifunga la piliIn control: Willian climbs on the back of Eto'o to celebrate his second goal
    Willian akimpongeza Eto'oSuper sub: Demba Ba converts from close-range to wrap up a 3-0 win for Chelsea
    Super sub: Demba Ba akifunga bao la tatuInstant impact: Ba celebrates his goal just six minutes after coming off the bench
    Ba akishangilia bao lake
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAIKALISHA BORUSSIA DORTMUND, ETO'O APIGA MBILI CHELSEA IKIUA WAJERUMANI...MESSI KAMA KAWA, AIPIGIA MBILI BARCA IKIINYANYASA AC MILAN ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top