• HABARI MPYA

    Saturday, November 30, 2013

    KIM POULSEN APANGUA KIKOSI STARS, DILUNGA BENCHI KESHO, CHUJI ATAANZA

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    KOCHA Mdenmark, Kim Poulsen anatarajiwa kuwa na marekebisho madogo katika kikosi chake cha kesho kitakachomenyana na Somalia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kutoka kile kilichocheza na Zambia juzi.
    Baada ya sare ya 1-1 na Zambia katika mchezo wa kwanza wa Kundi B juzi Uwanja wa Kenyatta, Machakos, kesho Uwanja wa Nyayo Nairobi, safu ya kiungo ya Stars itabadilika.
    Kesho benchi; Hassan Dilunga kesho ataanzia benchi Nyayo

    Kiungo chipukizi Hassan Dilunga ataanzia benchi na kumuachia nafasi mkongwe, Athumani Iddi ‘Chuji’- hiyo ni kwa mujibu wa mazoezi ya leo ya Stars Uwanja wa Chuo Kikuu cha Strathmore, Nairobi.
    Kipa Ivo Mapunda atasimama langoni akiendelea kulindwa na Himid Mao kulia, Erasto Nyoni kushoto, Said Morad na Kevin Yondan katikati, wakati kiungo wao mkabaji atakuwa Frank Domayo.
    Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Amri Kiemba watacheza pembeni juu huku wakimsaidia sana Chuji katikati na Elias Maguri na Mrisho Ngassa watacheza mbele ya lango la wapinzani.
    Athumani Iddi kushoto ataanza katikati pamoja na Frank Domayo kulia kesho Nyayo. CHINI: Sure Boy kulia na Erasto Nyoni kushoto wataanza pia.

    Kwa mujibu wa mazoezi ya leo, Stars kesho itatumia mipira mirefu kushambulia na ndiyo maana Chuji kaanzishwa kwa sababu ni mtaalamu wa kupiga pasi ndefu kwa mawinga na washambuliaji.
    Na hapa wazi Kim Poulsen anataka mabao mengi katika mchezo huo ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda Robo Fainali, kwani Somalia ni timu ambayo inaweza kufungwa na timu zote katika kundi hilo baada ya juzi kufungwa 2-0 na ‘Vitoto vya Burundi’.
    Stars itashuka dimbani kesho mchana kumenyana na Burundi wakati jioni Zambia itacheza na Burundi kwenye Uwanja huo huo wa Nyayo.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIM POULSEN APANGUA KIKOSI STARS, DILUNGA BENCHI KESHO, CHUJI ATAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top