• HABARI MPYA

    Sunday, November 10, 2013

    DIRISHA DOGO KUFUNGULIWA NOVEMBA 15

    Na Boniface Wambura, Ilala
    USAJILI wa wachezaji kwa dirisha dogo kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara unafunguliwa Novemba 15 mwaka huu na utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka huu.
    Kwa mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.
    Juma Kaseja amesaini Mkataba na Yanga na sasa atasajiliwa rasmi dirisha dogo litakapofunguliwa

    Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.
    Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.
    Matukio mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DIRISHA DOGO KUFUNGULIWA NOVEMBA 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top