YANGA SC imeingia Mkataba wa miaka miwili na Juma Kaseja, kipa maarufu nchini, aliyetemwa Simba SC mwishoni mwa msimu, kwa madai kiwango chake kimeshuka.
Kaseja ni kama hakuamini ametemwa Simba SC na akawa na subira kwa kutotaka kusaini timu nyingine, akiwasikilizia viongozi wake. Akawaonyesha bado ni wao kwa kuthubutu kwenda kufanya mazoezi na timu ya vijana ya klabu hiyo.
Alipojiridhisha Simba SC hawana haja naye, akairudia moja ya ofa alizopewa baada ya kutemwa Msimbazi- na hiyo si nyingine bali ni ya Yanga. Amepewa Sh. Milioni 40 na atakuwa anapata mshahara wa zaidi ya Sh. Milioni 1 kwa mwezi.
Yanga timu kubwa, atavuna marupurupu mengi na posho za migawo ya mechi- kwa kifupi furaha imerejea katika maisha yake. Na hakuna shaka, Kaseja ni kipa mzuri- kama kuna wakati kweli aliyumba, hiyo ni hali ya kawaida ambayo huwatokea wachezaji wengi duniani.
Baada ya kuingia Mkataba na Yanga, kinachofuata ni namna gani Kaseja ataishi na makipa ambao walimkimbia Simba kwa sababu alikuwa akiwaweka benchi, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ walio Jangwani kwa sasa.
Tayari baadhi ya vyombo vya habari vimekwishaanza kuandika Barthez atarudi Simba SC kwa sababu hataki kukaa timu moja na Kaseja. Kweli, Barthez na Dida waliondoka kwa wakati tofauti Simba SC kwenda kutafuta timu ambazo watakuwa wanadaka, Deo akaenda Mtibwa Sugar baadaye Azam na Ally akatangulia Yanga.
Hakukuwa na namna kwa wakati huo, Dida na Barthez hapana shaka walichukua uamuzi sahihi ambao umewasaidia katika maisha yao ya soka, kwa sababu uongozi wa Simba SC wakati huo ulikuwa unaamini lango lao haliwezi kuwa salama bila ya Kaseja.
Makipa wote watatu sasa umri umeenda kidogo na wamekutana tena katika timu moja- hiyo ndiyo unaambiwa hakuna anayeijua kesho yake itakuwaje. Wataishije? Hilo ndilo suala ambalo linawaumiza vichwa wapenzi wengi wa Yanga kwa sasa.
Wote ni makipa wazuri- na sasa inakumbushia mwaka 1993 Yanga SC walipokutana makipa watatu bora watupu, Sahau Kambi na Riffat Said ambao wote kwa sasa marehemu pamoja na Steven Nemes.
Marehemu Kambi ndiyo alikuwa katika siku zake za mwisho za soka na Nemes alikuwa mkongwe, wakati Riffat ndiyo alikuwa anaibuka. Nemes alikuwa kipa wa kwanza, lakini Riffat alikuwa anapewa nafasi pia kudaka. Kambi alistaafu baada ya msimu wa 1993.
Katika fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1993 Uwanja wa Nakivubo, mjini Kampala kati ya Yanga SC na wenyeji SC Villa, Nemes aliumia ndani ya dakika 10 na kocha Nzoyisaba Tauzany (marehemu) akamuinua marehemu Riffat kwenda kuchukua nafasi.
Waganda wakafurahia sana kwa kudhani kipa wa pili, atakuwa dhaifu, lakini alipoingia mtoto huyo wa Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad akafanya kazi nzuri, Yanga ikashinda 2-1 na kutwaa Kombe.
Nemes na Riffat waliishi pamoja hadi mwaka 1994, Yanga ilipovunja kikosi kufuatia kufungwa 4-1 na wapinzani wa jadi, Simba SC. Nemes ambaye sasa anaitwa Abdulmalik baada ya kusilimu akaenda Simba SC ambako alikutana na Mwameja Mohamed na Joseph Katuba, wote makipa wazuri na wanadakia timu ya taifa.
Walifanya kazi pamoja hadi mwaka 1997 Katuba alipokwenda Yanga SC na Mwameja Uingereza. Na wakati wote walikuwa wanaitwa pamoja timu ya taifa, makipa kutoka klabu moja.
Nakumbuka Pamba ya Mwanza wakati fulani ilikuwa ina makipa wawili wote wazuri, Madata Lubigisa na Paul Rwechungura na walifanya kazi pamoja. Yanga pia waliwahi kukutana makipa watatu wazuri watupu, Manyika Peter, Chachala Muya na Ismail Suma na wote walifanya kazi pamoja.
Hili ni jambo ambalo linawezekana na tangu enzi hizo makipa bora waliishi pamoja. Athumani Mambosasa na Omar Mahadhi ‘Bin Jabir’ (wote marehemu) walifanya kazi pamoja Simba SC miaka ya 1970, Hamisi Kinye alifanya kazi pamoja na Juma Mhina Yanga SC miaka ya 1980. Inawezekana.
Kikubwa tu ni kwamba, hawa vijana wanahitaji kuishi kwa akili zao na kutokubali kushikiwa akili na watu. Kaseja wa leo si yule wa miaka mitatu iliyopita kwamba anaweza kudaka peke yake msimu mzima, hapana. Kwa usalama wa kipaji chake, anahitaji kudaka na kupumzika na ili lango la klabu liwe salama, linahitaji kuwa na makipa wazuri angalau wawili.
Sioni tatizo Dida, Barthez kufanya pamoja, bali itategemea na busara ya mwalimu wa timu katika kuwafanya makipa wote hao wafurahie maisha Yanga SC.

.png)
0 comments:
Post a Comment