IMEWEKWA JUNI 4, 2013 SAA 8:50 MCHANA
KOCHA Jose Mourinho amewalenga wachezaji watano kuwasajili baada ya kurejea Chelsea kwa mara ya pili.
Wachezaji wa mwanzoni anaowataka wanafahamika ni washambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic, Manchester City, Edin Dzeko, sentahafu wa Porto, Eliaquim Mangala, Daniele De Rossi wa Roma na kiungo Mbrazil, Fernandinho wa Shakhtar Donetsk.
Mourinho pia ameweka wazi kumrejesha to Romelu Lukaku, baada ya kufanya vizuri msimu huu akiwa na West Brom ambako amefunga mabao 17, kwamba hataki atolewe kwa mkopo tena.

Jose Mourinho amesaini Mkataba wa miaka minne kurejea Chelsea, alipoondoka mwaka 2007

Sura mpya: Mourinho hataki Romelu Lukaku atolewe tena kwa mkopo waakti anamtaka na Daniele De Rossi (chini)

Kevin de Bruyne, ambaye ameomba kuuzwa moja kwa moja Borussia Dortmund baada ya kucheza kwa mkopo Werder Bremen, atakutana na kocha huyo mpya kabla ya kufikiwa uamuzi juu ya mustakabali wake.
Lakini Mourinho amesistiza hatafanya mabadiliko makubwa msimu huu, akisema: "Tunatakiwa kuimarisha timu, na ninaposema naimarisha timu, watu tayari wanafikia mamilioni mangapi Chelsea watatumia.
"Lakini ninaposema naimarisha timu nasema kuimarisha kwa kazi. Kazi yangu lazima iimarishe wachezaji na kuimarisha timu. Ikiwa sitafanya hivyo sitakuwa na furaha binafsi.
"Ikiwa baada ya hapo tutaimarisha timu kwa kununua wachezaji wachezaji wachache, itakuwa nzuri. Nataka kuanzia chini sifuri, nahitaji kufanya kazi ngumu tena na ujenga timu tofauti na ile niliyojenga wakati ule. Nataka kusahau kwamba nilikuwa bingwa hapa na ninataka niwe hamasa hiyo binafsi kama nipo hapa kwa mara ya kwanza,"alisema.

Anayetakiwa zaidi: Mshambuliaji wa Fiorentina, Stevan Jovetic

Beki wa Porto, Mfaransa Eliaquim Mangala (kushoto) anatakiwa pia

Kiungo Fernandinho alicheza dhidi ya Chelsea msimu uliopita akiwa Shakhtar


.png)