• HABARI MPYA

    Saturday, November 28, 2020

    KASEKE TENA, YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUJINAFASI KILELENI LIGI KUU TZ BARA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imejiweka sawa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya Azam FC wanaofuatia, ingawa wana mechi moja mkononi.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abel William wa Arusha, aliyesaidiwa na Sunday Komba wa Kilimanjaro na Hamdan Said wa Mtwara, bao pekee la Yanga SC limefungwa na kiungo Desu Kaseke dakika ya 33 akimalizia pasi ya Mburkinabe Yacouba Sogne.


    Huu ni ushindi wa pili mfululizo ukitokana na bao la Kaseke kwa pasi yule yule Yacouba baada ya ushindi wa 1-0 pia dhidi ya Azam FC katikati ya wiki, kufuatia sare tatu mfululizo 0-0 na Gwambina, 1-1 na Simba SC na 1-1 na Namungo FC.
    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Dodoma Jiji FC imeichapa Ihefu SC 3-0, mabao ya Seif Abdallah Karihe mawili dakika ya 32 na 55 na Augustino Samson dakika ya 44 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, wakati Mbeya City imelazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’/Abdallah Shaibu ‘Ninja’ dk70, Yassin Mustapha, Said Juma ‘Makapu’, Bakari Mwamnyeto, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Feisal Salum/Zawadi Mauya dk55, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke na Yacouba Sogne/Farid Mussa dk55. 
    JKT Tanzania; Joseph Ilunda, Michael Aidan, Hassan Twalib, Edson Katanga, Nurdin Mohammed, Jabir Aziz, Shaaban Mgandila, Hafidh Mussa, Daniel Lyanga, Adam Adam/Mohamed Rashid dk81 na Kelvin Nashon/Ally Bilal dk76. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEKE TENA, YANGA SC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 NA KUJINAFASI KILELENI LIGI KUU TZ BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top