• HABARI MPYA

    Saturday, July 14, 2018

    TFF YABADILI MFUMO WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imebadili kupitisha mfumo wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara juu ya timu za kushuka na kupanda.
    Na kuanzia msimu ujao FDL itachezwa katika makundi mawili yenye timu 12 na timu 1 kutoka kila kundi itapanda kwenda Ligi Kuu wakati timu zitakazoshika nafasi ya pili na ya tatu katika makundi yote zitacheza mtoano kwa mechi za nyumbani na ugenini.
    Taarifa ya TFF imesema kwamba washindi katika mechi hizo watacheza na timu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 katika Ligi Kuu kupata timu mbili zitakazocheza Ligi Kuu, huku timu mbili za nafasi ya 19 na 20 zikishuka daraja.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na wachezaji wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba Mei 19, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Timu hizo mbili za Ligi Kuu zilizoshika nafasi ya 17 na 18 kama zitapoteza michezo yao zitashuka Daraja kuungana na zilizoshika nafasi ya 19 na 20 na TFF imesema kwamba inafanya hivyo ili kuongeza ushindani wa Ligi Kuu, FDL na SDL. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YABADILI MFUMO WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top