• HABARI MPYA

  Saturday, July 14, 2018

  MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAREJESHWA…ITAANZA JUNI MWAKANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imekubaliana kurejesha michuano maarufu ya Kombe la Taifa. 
  Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari imesema kwamba mashindano ya Taifa Cup yatafanyika kati ya Juni na Julai kuanzia mwakani 2019.
  Pamoja na hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF imepitisha kuchezwa kwa mashindano ya Vijana U15 katika mtindo uliokuwa unatumika kwenye Copa Coca Cola wakati yale ya U17 yenyewe yatahusisha klabu za Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Daraja la Pili kwa pamoja. 
  Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) na Katibu wake, Wilfred Kidau (kushoto) 

  Nayo mashindano ya Kombe la Shirikisho yataanzia katika ngazi ya mkoa ambapo kila mkoa utakuwa na bingwa wake.
  Wakati huo huo: Rais wa TFF, Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Matagi Yasoda aliyefariki dunia juzi.
  Katika salamu zake za rambirambi, Rais wa TFF Ndugu Karia amesema mama Yasoda enzi za uhai wake alikuwa mwanamichezo mzuri hivyo aliyeshiriki katika shughuli mbalimbali za michezo hususani mpira wa Miguu.
  “Kifo cha mama Yasoda kimenishtua nilimfahamu kama mwanamichezo mzuri katika ngazi ya uongozi aliyeshiriki kikamilifu katika michezo,kwa niaba ya TFF natoa pole kwa familia,ndugu,jamaa,marafiki na familia ya michezo” alisema Rais wa TFF Ndugu Karia.
  Juliana Yasoda amefariki jana baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAREJESHWA…ITAANZA JUNI MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top