• HABARI MPYA

  Thursday, July 19, 2018

  KILIMANJARO QUEENS YAANZA VIBAYA KOMBE LA CHALLENGE…YACHAPWA 1-0 NA RWANDA

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  TIMU ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imeanza vibaya michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Rwanda Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. 
  Bao pekee la Nyigu wa kike wa Rwanda lililoizamisha Bara leo limefungwa na Kalimba Alice dakkika ya 34 katika mchezo huo. Michuano hiyo inashirikisha timu tano, nyingine ni Kenya, Uganda na Ethiopia.
  Mechi ya kwanza Uganda iliimiminia Kenya 1-0 hapo hapo Uwanja wa Nyamirambo. 
  Jumamosi Tanzania Bara itamenyana na Kenya, wakati Uganda itamenyana na Ethiopia. Bara watateremka tena uwanjani Jumatatu kumenyana na Uganda, siku ambayo Rwanda itamenyana na Ethiopia.

  Jumatano kutakuwa na mechi mbili pia, Kenya na Ethiopia na Uganda an Rwanda. Mechi za mwisho zitachezwa Ijumaa ya Julai 27, Tanzania Bara na Ethiopia na Rwanda na Kenys.
  Ikumbukwe Tanzania ndiyo mabingwa watetezi waliotwaa Kombe mwaka jana nchini Uganda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAANZA VIBAYA KOMBE LA CHALLENGE…YACHAPWA 1-0 NA RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top