• HABARI MPYA

  Friday, July 20, 2018

  JUMA KASEJA, MUSSA MGOSI WAITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA SOKA LA UFUKWENI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKONGWE Juma Kaseja na Mussa Hassan Mgosi waliokuwa kuwika kwenye soka ya kimataifa nchini wamejumuishwa kwenye kikosi cha ya taifa ya soka ya ufukweni. 
  Kaseja ambaye amesajiliwa na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara akitokea Kagera Sugar ya Bukoba na Mgosi ambaye kwa sasa anachezea Dodoma FC ya Daraja la Kwanza wameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya soka la ufukweni.
  Kocha Mkuu wa timu hiyo, Boniface Pawasa aliyewahi kucheza na wote, Kaseja na Mgosi klabu ya Simba na timu ya taifa, amesema kwamba kikosi cha timu ya taifa ya soka la ufukweni kitaanza mazoezi kesho kwenye fukwe za Coco Beach mjini Dar es Salaam. 

  Juma Kaseja amesajiliwa na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara akitokea Kagera Sugar ya Bukoba

  Pawasa amesema kwamba amewachukua Kaseja na Mgosi kutokana na uzoefu wao kwenye soka, lakini wachezaji wengine wote amewateua baada ya kufanya vizuri kwenye michuano maalum ya Vyuo vya Elimu ya Juu soka la ufukweni.
  “Tunatarajia kuanza mazoezi kesho kwenye Fukwe za Coco Beach kwa wachezaji tuliowaita katika kikosi cha timu ya taifa ya Beach Soccer na tutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Zanzibar ili kupata wachezaji wa kuongeza kikosini kutoka upande huo wa pili wa Muungano wa nchi yetu,”amesema Pawasa.
  Baada ya uteuzi huo wa mwisho wa timu ya taifa ya ufukweni itakwenda Afrika Kusini kati ya Agosti 7 na 9, mwaka huu kwa ajili ya mchezo na wenyeji, kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 21 na 23 kuwania timeit ya Fainali za Afrika za soka la ufukweni.
  Wachezaji wengine walioyeuliwa kwenye kikosi hicho cha awali ni Khalifa Mgaya, Rajabu Ghana, Ibrahim Abdallah, Damian Paul, Juma Ibrahim, Kashiru Salum, Samuel Salonge, Rolland Msongo, Gama David Yenas, Ramadani Nganda, Shaaban Dola, Ally Rabbi, Jarufu Joseph, Mbwana Mshindo, Alfa Tandise, Yahaya Turbo, Deo Masanja, Attidius Ishengoma, Simba Adolph, Ramadhan Ally na Kudra Omar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JUMA KASEJA, MUSSA MGOSI WAITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA SOKA LA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top