Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
KIUNGO chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Said Hamisi Ndemla leo amepewa adhabu ya kupiga pushapu baada ya kuunganishia juu ya lango krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa.
Ndemla, kiungo wa Simba SC ya Tanzania alipewa adhabu hiyo na kocha Mholanzi, Mart Nooij baada ya kupiga mpira juu ya lango akiwa umbali wa mita nane katika mazoezi yaliyofanyika viwanja vya Michezo vya Rustenburg mjini hapa.
Taifa Stars ipo katika matayarisho ya mwishoni kuelekea mchezo wake wa kwanza wa COSAFA 2015 dhidi ya Swaziland Jumatatu.
Katika mazoezi ya leo, Nooij alikuwa anawafundisha wachezaji wake mipango ya kutengeneza nafasi na kufunga mabao.
Nooij ambaye siku mbili zilizopita timu yake ilifanya mazoezi Uwanja Olimpia Park, leo alikuwa akiwaelekeza wachezaji wake namna ya kusaka mabao.
Alikuwa akiwaelekeza vijana wake namna ya kupanga shambulizi hadi kufika langoni kwa wapinzani na kufunga.
Na katika mfumo huo, wachezaji wa nne wote wa mbele walikuwa wanapishana nafasi, wakati mwingine wengine wakienda pembeni na kurudi katikati wakipishana.
Unaonekana kuwa mfumo mzuri wa kusuka nafasi za mabao, iwapo wachezaji watauelewa vizuri na kuweza kuufanyia kazi uwanjani.
Ni mfumo ambao mipira inayowapita washambuliaji, viungo wanatakiwa kuifuatilia kumalizia kwa mashuti makali.
Wote Mrisho Ngassa, John Bocco, Juma Luizo na Ibrahim Hajib walionyesha umahiri wa kufunga na kupiga krosi.
Viungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mwinyi Kazimoto, Hassan Dilunga na Said Ndemla walikuwa makini katika kumalizia mipira inayowapita washambuliaji. Lakini Ndemla, alipokosea mara moja baada ya kupiga juu kabisa ya lango, alipigishwa pushapu na tangu hapo akajirekebisha.
Kocha Msaidizi, Salum Mayanga alikuwa katika lango lingine akiinoa safu ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya aina tofauti, hususan ya kutokea pembeni kutokana na mipira ya kona na krosi.
Stars iliyopangwa Kundi A katika COSAFA, inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza Jumatatu wa Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace dhidi ya Swaziland.
Mbali na Swaziland, timu nyingine katika kundi la Taifa Stars ni Lesotho na Madagascar, wakati Kundi B lina timu za Shelisheli, Namibia, Zimbabwe na Mauritius.

![]() |
| Said Ndemla akipiga pushapu, adhabu aliyopewa na kocha wake, Mart Nooij baada ya kupiga juu ya lango akiwa umbali wa mita nane |
Katika mazoezi ya leo, Nooij alikuwa anawafundisha wachezaji wake mipango ya kutengeneza nafasi na kufunga mabao.
Nooij ambaye siku mbili zilizopita timu yake ilifanya mazoezi Uwanja Olimpia Park, leo alikuwa akiwaelekeza wachezaji wake namna ya kusaka mabao.
Alikuwa akiwaelekeza vijana wake namna ya kupanga shambulizi hadi kufika langoni kwa wapinzani na kufunga.
Na katika mfumo huo, wachezaji wa nne wote wa mbele walikuwa wanapishana nafasi, wakati mwingine wengine wakienda pembeni na kurudi katikati wakipishana.
Unaonekana kuwa mfumo mzuri wa kusuka nafasi za mabao, iwapo wachezaji watauelewa vizuri na kuweza kuufanyia kazi uwanjani.
Ni mfumo ambao mipira inayowapita washambuliaji, viungo wanatakiwa kuifuatilia kumalizia kwa mashuti makali.
Wote Mrisho Ngassa, John Bocco, Juma Luizo na Ibrahim Hajib walionyesha umahiri wa kufunga na kupiga krosi.
![]() |
| Ndemla alijivuta vizuri wakati krosi ya Mrisho Ngassa (hayupo pichani) inakuja, lakini akapiga juu kabisa. Kulia ni Mwinyi Kazimoto |
Viungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mwinyi Kazimoto, Hassan Dilunga na Said Ndemla walikuwa makini katika kumalizia mipira inayowapita washambuliaji. Lakini Ndemla, alipokosea mara moja baada ya kupiga juu kabisa ya lango, alipigishwa pushapu na tangu hapo akajirekebisha.
Kocha Msaidizi, Salum Mayanga alikuwa katika lango lingine akiinoa safu ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya aina tofauti, hususan ya kutokea pembeni kutokana na mipira ya kona na krosi.
Stars iliyopangwa Kundi A katika COSAFA, inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza Jumatatu wa Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace dhidi ya Swaziland.
Mbali na Swaziland, timu nyingine katika kundi la Taifa Stars ni Lesotho na Madagascar, wakati Kundi B lina timu za Shelisheli, Namibia, Zimbabwe na Mauritius.

.png)
0 comments:
Post a Comment