NAUHESHIMU uwezo wa kocha Mserbia, Goran Kopunovic na ni aina ya makocha ambao binafsi ninawakubali mno.
Nawapenda sana makocha wanaoingia uwanjani na kufundisha kwa nadharia na vitendo, kuliko wale wanaoweka mikono mgongoni baada ya kutoa maelekezo.
Goran anatoa maelekezo, anatoa mifano na mchezaji akikosea, anamuita anamuelekeza, hadi anaelewa.
Ni kocha fulani, ambaye kama Simba SC watamvumilia, watakuja kujivunia mno baadaye.
Nasema kama watamvumilia kwa sababu, wakati mwingine matokeo mazuri, au mabaya hutokana na bahati, mbaya au nzuri.
Jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba mikataba yao ya sasa waliyoingia na wachezaji wao, inawapa fursa ya kuwatema bila malipo, iwapo watashuka viwango.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY katika mahojiano maalum juzi Dar es Salaam, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba baada ya kuona wanapata hasara kutokana na wachezaji wazembe, wakalazimika kutengeneza mikataba salama zaidi kwao.
“Sisi kama klabu tunasajili mchezaji ili atusaidie na ndiyo maana tunatumia fedha nyingi, haswa kwa hawa wachezaji wa kigeni. Lakini unamleta mtu katika timu anashindwa kufanya juhudi za kuisaidia timu,”.
“Ukisema umuache ili usajili mwingine, tena bila kujali kama ulimlipa fedha nyingi kiasi gani, anataka alipwe na fidia ya mishahara ya kipindi chote kilichobaki cha Mkataba aliosaini.
Na tumeingia hasara za namna hiyo nyingi tu. Kwanza ile tu kumsajili mchezaji kwa Mkataba wa miaka miwili kwa mfano, halafu baada ya miezi sita unaamua kumuacha, pekee ni hasara kubwa. Lakini unapomuacha anakushitaki hadi FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) umlipe fedha zaidi,”amesema Poppe.
Kutokana na hali hiyo, Poppe amesema kwamba walichimba zaidi FIFA kuhusu namna ya kuepukana na matatizo ya aina hiyo, wakagundua dawa ni kuboresha mikataba,”.
“Iko wazi hata FIFA, unapomsajili mchezaji katika Mkataba mnaandikiana kabisa, kama akishindwa kuonyesha uwezo na kocha akathibitisha, basi Mkataba utavunjwa bila malipo ya ziada,”amesema.
Poppe amewataka wachezaji wote wa Simba SC kuzingatia hilo na kuhakikisha wanakuwa katika viwango vizuri wakati wote ili waisaidie timu, vinginevyo ripoti ya kocha ikidhihirisha mchezaji ameshuka kiwango, ataachwa bila fidia.
“Na wao wanalijua hilo, kwa sababu katika Mikataba yao hiyo ipo. Sasa sisi tutasubiri ripoti ya mwalimu tu, akituambia mchezaji huyo ameshuka kiwango kuanzia asilimia 30 tutamuacha na ataondoka bila malipo ya ziada,”amesema.
Sitaki kujadili kuhusu mikataba, nataka kuzungumzia mpango wa Simba SC kuwaacha wachezaji ambao hawataonyesha umuhimu katika timu.
Ni jambo ambalo huwezi kupinga, klabu inasajili mchezaji ili asaidie timu kushinda mataji. Popote duniani, mchezaji ambaye hana msaada katika timu huachwa. Simba SC wako sahihi katika hili.
Lakini pamoja na ukweli huo, Simba SC wanatakiwa kufanya tathmini za kina juu ya wachezaji wao, kabla ya kufikia uamuzi wa kuwatema.
Mfano kwa sasa wachezaji wa kigeni wa SImba SC ambao wote ni Waganda, ni mabeki Juuko Murushid, Joseph Owino na washambuliaji Emmanuel Okwi, Dan Sserunkuma na Simon Sserunkuma.
Murushid na Okwi ndiyo wachezaji pekee ambao kwa fikra za viongozi wa Simba SC ndio wapo salama, lakini akina Sserunkuma na Owino lolote linaweza kutokea.
Dan Sserunkuma amesajiliwa msimu huu kutoka Gor Mahia ya Kenya ambako misimu yote miwili iliyopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Lakini pia, Dan amesajiliwa Simba SC akiwa mshambuliaji wa timu ya taifa Uganda na ndiye alikuwa tegemeo la safu ya ushambuliaji ya The Cranes mwaka juzi nchini Kenya katika CECAFA Challnge.
Sina shaka kuhusu uwezo wa Dan katika kufunga, lakini nakubali hajawa na mwanzo mzuri Simba SC. Simon ni mwanasoka kijana mdogo anayeinukia vizuri.
Vyombo vya habari nchini Uganda wakati fulani vilikuwa vinamsifia kama mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu, ambaye hajawahi kutokea katika ardhi ya nchi hiyo.
Lakini naye hajawa na mwanzo mzuri- Msimbazi, kiasi kwamba yeye na Dan na Owino wanatajwa katika orodha ya wachezaji ambao wanaweza kuachwa mwishoni mwa msimu.
Sitaki kuwalekeza viongozi wa Simba SC nini cha kufanya- ila nataka kuwaambia tu si wachezaji wote huingia katika timu mpya na kuanza kung’ara moja kwa moja.
Kwa kiasi kikubwa mchezaji mpya anaweza kuanza kuonyesha cheche katika msimu wa pili baada ya kuzoea mazingira. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Okwi wakati anasajiliwa kutoka Uganda, msimu wa kwanza ‘alionekana si lolote’.
Lakini baada ya misimu miwili, Tanzania ilimtambua Okwi ni nani.
Imekuwa desturi ya Simba SC kuwaacha wachezaji baada ya muda mfupi tu, kwa kuwa hawajaonyesha cheche. Naamini Simba SC imepoteza wachezaji wengi wazuri kwa staili hiyo, achilia mbali fedha za kusajili na kuvunja mikataba.
Wakati umefika sasa viongozi wa Simba SC waamue kuwavutia subira wachezaji wapya, angalau kuanzia msimu wa pili ndipo wafikirie kuwatema iwapo hawatabadilika.

.png)
0 comments:
Post a Comment