Na Mwandishi wetu, MOSHI
MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na vilabu vya, Ajax na Balcelona, gwiji Johan Cruyff amewasili jana majira ya saa 4:45 za asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo, Cruyff akiwa ameambatana na familia yake alipokelewa na Rayco Garcia, mratibu wa ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania watakao cheza mechi ya kirafiki dhidi ya wakongwe wa soka hapa nchini jumamosi ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Cruyff alisema anafurahi kufika Tanzania kwa mara ya kwanza na kwamba amefurahia hali ya hewa ya Joto ukilinganisha na nchi anayotoka ambayo kwa sasa ni msimu wa baridi.
Alisema ana matarajio makubwa baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania ikiwemo kuona wanyama wa aina mbalimbali katika hifadhi ya taifa ya Serengeti pamoja na kutembelea fukwe za bahari katika kisiwa cha Zanzibar kabla ya mchezo huo wa kirafiki.
“Nasikia furaha kufika Tanzania, na hali ya hewa ni nzuri, hali ya joto, tunategemea kutembelea maeneo mengi ya vivutio, tunaenda kutizama
wanyama katika hifadhi ya Serengeti na baadae kutembea fukwe huko Zanzibar, tunategemea kuona vitu vingi vizuri.”alisema Cruyff.
Kuhusu mchezo wa Jumamoshi ,Cruyff alisema mashabiki wategemeee burudani toka kwa wakongwe hao wa Barcelona na kwamba mchezo huo hautakuwa wa ushindani isipokuwa wataonesha burudani ambayo ni matarajio ya wengi.
“Kitu cha kwanza ni kwamba mashabiki watapata Burudani, hatutacheza ili kushinda ingawaje tutapenda kushinda, lakini kikubwa ni kutoa burudani kwa mashabiki,wafike tu uwanjani kufurahia mchezo”alisema Cruyff.
Cruyff ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’O ,1971,1973 na 1974 aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma katika mazoeizi ni
kuzingatia maelekezo ya walimu ili kujenga morali ya timu na wachezaji kwa ujumla.
“Naweza sema kwa wachezaji pekee ,wanapaswa kufanya mazoezi kwa bidii, wajaribu kujiweka vizuri kila mara na kitu kizuri katika michezo
ni umoja wa timu, mkishinda mnashinda pamoja na mkipoteza mnapoteza pamoja” alisema Cruyff.
Kuelekea katika Pambano la Jumamosi tayari waratibu wa mashindano hayo walisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba baadhi ya wachezaji wa Barcelona watakao shuka uwanjani siku hiyo ni pamoja na wakongwe
Edaga Davis ,Deco,Patrick Kluivert na Simao Sabrosa.
HISTORIA FUPI YA CRUYFF.
Mdachi Hendrik Johannes Cruijff alizaliwa Aprily 25 mwaka 1947 katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi, akajulikana kama Johan Cruyff ambaye hadi sasa ni meneja wa klabu ya Catalonia ya nchini Hispania.
Cruyff ni miongoni mwa wachezaji maarufu walio anzisha falsafa ya "Total Football"ambayo ilienea kote duniani hatua iliyopelekea kuwa mmoja wa wachezaji wenye sifa kubwa katika historia ya soka duniani.
Cruyff alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za kombe la dunia la Fifa ,mwaka 1974 ambapo alifanikiwa kupata zawadi
ya mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa mashindano. Amewahi kuwa kocha wa vilabu vya Ajax na Barcelona kwa nyakati tofauti.
MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na vilabu vya, Ajax na Balcelona, gwiji Johan Cruyff amewasili jana majira ya saa 4:45 za asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo, Cruyff akiwa ameambatana na familia yake alipokelewa na Rayco Garcia, mratibu wa ziara ya wachezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania watakao cheza mechi ya kirafiki dhidi ya wakongwe wa soka hapa nchini jumamosi ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Cruyff alisema anafurahi kufika Tanzania kwa mara ya kwanza na kwamba amefurahia hali ya hewa ya Joto ukilinganisha na nchi anayotoka ambayo kwa sasa ni msimu wa baridi.
![]() |
| Johan Cruyff baada ya kuwasili KIA leo |
“Nasikia furaha kufika Tanzania, na hali ya hewa ni nzuri, hali ya joto, tunategemea kutembelea maeneo mengi ya vivutio, tunaenda kutizama
wanyama katika hifadhi ya Serengeti na baadae kutembea fukwe huko Zanzibar, tunategemea kuona vitu vingi vizuri.”alisema Cruyff.
Kuhusu mchezo wa Jumamoshi ,Cruyff alisema mashabiki wategemeee burudani toka kwa wakongwe hao wa Barcelona na kwamba mchezo huo hautakuwa wa ushindani isipokuwa wataonesha burudani ambayo ni matarajio ya wengi.
“Kitu cha kwanza ni kwamba mashabiki watapata Burudani, hatutacheza ili kushinda ingawaje tutapenda kushinda, lakini kikubwa ni kutoa burudani kwa mashabiki,wafike tu uwanjani kufurahia mchezo”alisema Cruyff.
Cruyff ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’O ,1971,1973 na 1974 aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma katika mazoeizi ni
kuzingatia maelekezo ya walimu ili kujenga morali ya timu na wachezaji kwa ujumla.
“Naweza sema kwa wachezaji pekee ,wanapaswa kufanya mazoezi kwa bidii, wajaribu kujiweka vizuri kila mara na kitu kizuri katika michezo
ni umoja wa timu, mkishinda mnashinda pamoja na mkipoteza mnapoteza pamoja” alisema Cruyff.
Kuelekea katika Pambano la Jumamosi tayari waratibu wa mashindano hayo walisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba baadhi ya wachezaji wa Barcelona watakao shuka uwanjani siku hiyo ni pamoja na wakongwe
Edaga Davis ,Deco,Patrick Kluivert na Simao Sabrosa.
![]() |
| Johan Curyff (kulia) alikuwa mwenye furaha sana leo baada ya kuwasili Kilimanjaro |
HISTORIA FUPI YA CRUYFF.
Mdachi Hendrik Johannes Cruijff alizaliwa Aprily 25 mwaka 1947 katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi, akajulikana kama Johan Cruyff ambaye hadi sasa ni meneja wa klabu ya Catalonia ya nchini Hispania.
Cruyff ni miongoni mwa wachezaji maarufu walio anzisha falsafa ya "Total Football"ambayo ilienea kote duniani hatua iliyopelekea kuwa mmoja wa wachezaji wenye sifa kubwa katika historia ya soka duniani.
Cruyff alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za kombe la dunia la Fifa ,mwaka 1974 ambapo alifanikiwa kupata zawadi
ya mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa mashindano. Amewahi kuwa kocha wa vilabu vya Ajax na Barcelona kwa nyakati tofauti.

.png)
0 comments:
Post a Comment