• HABARI MPYA

    Tuesday, November 05, 2013

    WENGER AWAAMBIA ARSENAL KUHUSU NDOA MPYA NA YEYE, WASUBIRI SUBIRI KIDOGO...BADO ANAKUNA KICHWA

    KOCHA Arsene Wenger atawataka Arsenal wawe na subira juu ya mustakabali wake katika klabu hiyo hadi watakapofuzu kwa hatua ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Pamoja na hayo, Arsenal wanajiamini kwamba Wenger atasaini Mkataba a kuendelea kufanya kazi ambao utamuwezesha kupata Pauni Milioni 7.5 kwa mwaka Mfaransa huyo.
    Wenger, ambaye ametimiza miaka 64 mwezi uliopita, hakutaka Mkataba wake ujadiliwe katika kipindi hiki cha ratiba ngumu kwa timu.
    Anasubiri: Arsene Wenger anasubiri hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa iishe ndipo mjadala wa Mkataba mpya uchukue nafasi
    Hopeful: Arsenal are confident that Wenger will sign an extension to his existing £7.5million a year deal
    Matumaini: Arsenal wanajiamini kwamba Wenger atasaini Mkataba wa Pauni Milioni 7.5 ili kubaki Arsenal

    Arsenal inakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Borussia Dortmund kesho Jumatano kabla ya kusafiri hadi Manchester kwa ajili ya kumenyana na mabingwa watetezi, United Uwanja wa Trafford Jumapili.
    Wapo katika kundi gumu kwenye Ligi ya Mabingwa pamoja na Marseille na Napoli na Wenger anatarajiwa kusubiri hadi baada ya hapo ndipo ataamua kuhusu mustakabali wake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AWAAMBIA ARSENAL KUHUSU NDOA MPYA NA YEYE, WASUBIRI SUBIRI KIDOGO...BADO ANAKUNA KICHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top