KOCHA David Moyes amesema winga Adnan Januzai lazima alindwe na marefa baada ya Sascha Riether kuwa mchezaji wa kwanza kuadhibiwa chini ya sheria mpya baada ya marefa kutoona tukio uwanjani .
Mshambuliaji huyo kinda alikuwa alichezewa rafu na beki huyo wa Fulham, United ikishinda 3-1 Uwanja wa Craven Cottage Jumamosi.
Refa Lee Probert na wasaidizi wake hawakuona tukio hilo wakati linatokea, lakini marudio ya picha za video yanaonyesha vizuri.

Ulinzi: David Moyes amesema Januzaj anahitaji kulindwa na marefa

Umewaona: Wachezaji wa Manchester United wakiwa kwenye Uwanja wa Estadio Anoeta kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Sociedad usiku wa leo

Anajifunza: Moyes amesema kinda huyo anajifunz namna ya kukabiliana na rafu

Adhabu: Sascha Riether ameadhibiwa na FA kwa tukio hili

Kama Messi: Januzaj anastahili kulindwa zaidi na marefa, amesema Moyes
Na kwa sababu huyo, beki huyo wa pembeni ameadhibiwa na FA kwa kufungiwa mechi tatu.
Inamaanisha Riether anakuwa mchezaji wa kwanza kuadhibiwa chini ya sheria mpya ya FA, kumuadhibu mchezaji ambaye alifanya kosa lakini halikuonekana kwa marefa wakat wa mechi.



.png)
0 comments:
Post a Comment