• HABARI MPYA

    Tuesday, November 12, 2013

    WENGER ATAKA KUMTIA PINGU YA MIAKA MINNE MERTESACKER 'AFIE' ARSENAL

    KLABU ya Arsenal inajiamini beki wake tegemeo, Per Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa muda mrefu.
    Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani juu ya vipengele vya Mkataba na inafahamika mazungumzo yanaendelea vizuri.
    Mertesacker amedhihirisha yeye ni mwamba wa safu ya ulinzi ya The Gunners akitengeneza ukuta mgumu wa mabeki wanne akicheza sambamba na Laurent Koscielny.
    Mwamba: Arsenal inaamini kwamba Per Mertesacker atasaini Mkataba mpya
    Committed: Manager Arsene Wenger wants to tie Mertesacker down to a four-year contract
    Majukumu: Kocha Arsene Wenger anataka kumfunga pingu Mertesacker ya Mkataba wa miaka minne

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza miezi 18 katika Mkataba wake wa sasa, ambao unamfanya alipwe mshahara wa Pauni 65,000 kwa wiki na kocha Arsene Wenger anataka mustakabali wake ukamilishwe haraka iwezekanavyo. 
    Na ikiwa mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa, Mertesacker atasaini Mkataba mpya wa miaka minne, ambao utahusisha kupanda kwa maslahi yake kabla ya mwisho wa mwaka huu.
    Baada ya kuwa mwanzo na mgumu Uwanja wa Emirates, hatimaye beki huyo wa nguvu wa kati amefanikiwa kuteka hisia za mashabiki wa klabu hiyo ya London Kaskazini- akifanya kazi nzuri mwanzoni mwa msimu huu.
    Steady: After a shaky start to his Arsenal career the German has become a mainstay
    Mkali kweli: Baada ya mwanzo mgumu Arsenal, beki huyo Mjerumani sasa mambo yanamuendea vizuri Emirates
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER ATAKA KUMTIA PINGU YA MIAKA MINNE MERTESACKER 'AFIE' ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top