RAIS wa FIFA, Sepp Blatter alizomewa ile mbaya jana Uwanja wa Santiago Bernabeu wakati Cristiano Ronaldo anafunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociadad kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
Mashabiki wa Real Madrid walikuwa wakimzomea Blatter aliyemkandia Ronaldo hivi karibuni na kumfagilia Lionel Messi wa Barcelona.
Na wakawa wanamuimba Ronaldo Ballon d' Or, maana yake anastahli kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia. Ronaldo alifunga dakika ya 12, 26 kwa penalti na 76, wakati mabao mengine ya Real yalifungwa na Benzema dakika ya 18 na Khedira dakika ya 36. Bao la kufutia chozi la wapinzani wao lilifungwa na Griezmann dakika ya 61.
Ronaldo sasa amefunga mabao tisa katika mechi nne zilizopita na anaongoza kwa mabao La Liga. Amefunga mabao 62 mwaka huu na sasa amefikisha hat-tricks 19 katika Ligi ya Hispania.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: López, Carvajal, Arbeloa, Alonso/Illarramendi dk70, Varane, Pepe, Khedira/Isco dk77, Modric, Benzema/Morata dk83, Bale na Ronaldo.
Real Sociedad: Bravo, Martínez/Ansotegi dk59, José Ángel, Elustondo/Zurutuza dk45, González, Iñigo Martínez, Vela, Bergara, Seferovic/De la Bella dk45, Xabi Prieto na Griezmann.
Kiwango tofauti: Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick ya 19 La Liga jana akiiongoza Real Madrid kuirarua 5-1 Real Sociedad


Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself




.png)
0 comments:
Post a Comment