• HABARI MPYA

    Wednesday, November 06, 2013

    MBEYA CITY WAJA DAR NA MASHABIKI 200 KUIVAA AZAM KESHO CHAMAZI

    Na Zaituni Kibwana, Sinza 
    KIKOSI cha Mbeya City kinachonolewa na Juma Mwambusi kimekuja Dar es Salaam na mashabiki 200 kwa mabasi maalum kwa ajili ya kuwapa sapoti kwenye  mechi dhidi ya Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mechi hiyo imekuwa gumzo kwa sasa baada ya timu hizo kuwa na pointi 26 kila mmoja huku Azam ikiwa juu kileleni kwa idadi kubwa ya mabao.
    Mashabiki 200 wa Mbeya City wamekuja Dar es Salaam

    Mwenyekiti wa timu hiyo, Mussa Mapunda alisema kuwa mashabiki hao mara baada ya kufika watatembelea hospitali yoyote ya serikali kwa ajili ya kuwafariki wagonjwa.
    Akizungumzia mechi hiyo mwenyekiti huyo alisema kuwa wamedhibiti hujuma za ndani ya uwanja na nje ili kuhakikisha wanaibuka na pointi 3 muhimu.
    “Tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi na sisi tuna rekodi nzuri ya kuhakisha tunaibuka na ushindi kwenye mechi za nje hivyo Azam wajiandae na kichapo,”alisema
    Alisema kuwa watapokea matokeo yoyote yatakaotokea kwenye mechi hiyo na wakishinda na kukaa kileleni hakuna wa kuwatoa.
    “Tuna jeuri ya kushinda mechi hiyo kwa kuwa tuna kikosi kinachotupa matumaini, hivyo tukikaa kileleni hakuna wa kutushusha,”alisema.
    Alimaliza kwa kuwataka waamuzi wa mchezo huo kutumia sheria 17 za soka na kupatikana mshindi wa hali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY WAJA DAR NA MASHABIKI 200 KUIVAA AZAM KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top