• HABARI MPYA

    Wednesday, November 06, 2013

    DOGO ABUU HASHIMU 'APINDUA' VIGOGO LANGO LA SIMBA SC

    Na Mahmoud Zubeiry, Taifa
    KIPA kinda wa Simba SC aliyepandishwa kutoka timu B, Abuu Hashimu nyota yake imeendelea kung’ara baada ya leo tena kuanzishwa katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ashanti United inayoanza saa 10:00 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa Abuu katika Ligi Kuu tangu aanze kudaka katika mechi na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga mwezi uliopita akimpokea kipa namba moja wa timu hiyo, Mganda Abbel Dhaira aliyeumia dakika ya 35. 
    Abuu Hashimu sasa anaelekea kuwa kipa namba moja Simba SC

    Abuu alimaliza dakika 65 za mechi hiyo bila kufungwa timu hizo zikitoka sare ya bila kufungana, lakini katika mchezo uliofuata dhidi ya Azam FC alirudi benchi, Dhaira akianza tena na Simba kufungwa 2-1.
    Kocha wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alimuanzisha Abuu katika mchezo uliopita wa timu hiyo dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba na akafungwa kwa penalti dakika za mwishoni timu hizo zikitoka sare ya 1-1.
    Na leo Dhaira anaanzia benchi wakati kipa aliyesajiliwa kwa mamilioni kutoka Kagera Sugar, Andrew Ntalla anaendelea kuwa mtazamaji jukwaani.
    Kwa kiasi kikubwa udakaji wake anamuiga Juma Kaseja, kipa aliyeidakia timu hiyo tangu mwaka 2003 kabla ya kutemwa mwishoni mwa msimu uliopita.
    Abuu ndiye kipa aliyeidakia Simba B hadi ikatwaa Kombe la Banc ABC mwaka jana ikizifunga timu nzuri zilizotumia nyota wake wa Ligi Kuu kama Azam FC na Mtibwa Sugar.
    Kikosi cha Simba SC kitakachomenyana na Ashanti ni; Abuu Hashimu, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Gilbert Kaze, Hassan Hatibu, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Henry Joseph, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Amri Kiemba, wakati benchi wapo Dhaira, William Lucian ‘Gallas’, Omar Salum, Hassan Isihaka, Edward Christopher, Said Ndemla na Ramadhani Chombo ‘Redondo’.  a
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DOGO ABUU HASHIMU 'APINDUA' VIGOGO LANGO LA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top