• HABARI MPYA

    Saturday, November 09, 2013

    KUBALI USIKUBALI BONGO HII HAKUNA MWANASOKA MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUCHEZEA MPIRA KAMA HUYU DADA

    Hadhara Charles ni binti mwenye kipaji cha hali ya juu ya kuchezea mpira ambaye hata hivyo hawezi kucheza soka ya ushindani kutokana na matatizo ya kiafya. Binti huyo amekuwa akialikwa kwenye hafla nyingi kubwa za kitaifa za michezo kuonyesha utundu wake na jana usiku alikuwepo kwenye ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam katika hafla ya tuzo za Wanasoka ya gazeti la Mwanaspoti. Habari njema ni kwamba, gazeti hilo lilitambua kipaji chake kwa kumpa tuzo maalum juu ya kipaji chake. 




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUBALI USIKUBALI BONGO HII HAKUNA MWANASOKA MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUCHEZEA MPIRA KAMA HUYU DADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top