Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kipre Herman Tchetche amefufua matumaini ya kutetea kiatu chake cha dhahabu, baada ya kufikisha mabao saba.
Mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast, jana aliifungia Azam FC bao moja katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
Kipre anayecheza timu moja na pacha wake, kiungo Kipre Michael Balou, sasa anazidiwa mabao mawili na mchezaji anayeongoza, Mrundi Amisi Tambwe wa Simba SC mwenye mabao tisa.
Kipre pia anazidiwa bao moja na mchezaji anayeshika nafasi ya pili, Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga SC, wakati pia analingana na Juma Luizio wa Mtibwa Sugar mwenye mabao saba pia.
Elias Maguri wa Ruvu Shooting ana mabao sita sawa na Themi Felix wa Kagera Sugar, wakati Mrisho Ngassa ana mabao matano sawa na Didier Kavumbangu anayecheza naye Yanga SC na Tumba Swedi wa Ashanti United, ambaye ndiye beki mwenye mabao mengi zaidi msimu huu hadi sasa.
WAFUNGAJI WA MABAO LIGI KUU:
JINA TIMU MABAO
Amisi Tambwe Simba SC 9
Hamisi Kiiza Yanga SC 8
Juma Luizio Mtibwa 7
Kipre Tchetche Azam FC 7
Elias Maguri Ruvu Shoot 6
Themi Felix Kagera 6
Mrisho Ngassa Yanga SC 5
Tumba Swedi Ashanti 5
D. Kavumbangu Yanga SC 5

![]() |
| Kipre Tchetche akiwa na tuzo yake ya ufungaji bora msimu uliopta. Kulia ni Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom, Kevin Twisa na kushoto Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara |
Kipre pia anazidiwa bao moja na mchezaji anayeshika nafasi ya pili, Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga SC, wakati pia analingana na Juma Luizio wa Mtibwa Sugar mwenye mabao saba pia.
Elias Maguri wa Ruvu Shooting ana mabao sita sawa na Themi Felix wa Kagera Sugar, wakati Mrisho Ngassa ana mabao matano sawa na Didier Kavumbangu anayecheza naye Yanga SC na Tumba Swedi wa Ashanti United, ambaye ndiye beki mwenye mabao mengi zaidi msimu huu hadi sasa.
WAFUNGAJI WA MABAO LIGI KUU:
JINA TIMU MABAO
Amisi Tambwe Simba SC 9
Hamisi Kiiza Yanga SC 8
Juma Luizio Mtibwa 7
Kipre Tchetche Azam FC 7
Elias Maguri Ruvu Shoot 6
Themi Felix Kagera 6
Mrisho Ngassa Yanga SC 5
Tumba Swedi Ashanti 5
D. Kavumbangu Yanga SC 5

.png)
0 comments:
Post a Comment