• HABARI MPYA

    Monday, November 04, 2013

    CARLOS VELA AMTIA NDIMU CHICHARITO, AMUAMBIA; "KAMA MAN UTD HAWAKUPANGI ONDOKA ZAKO, WEWE LULU ULAYA"

    MSHAMBULIAJI Javier Hernandez 'Chicharito' amezua hofua ndani ya Manchester United kuhusu mustakabali wake, baada ya kujibu katika Twitter habari kuhusu kuondoka katika timu hiyo iwapo ataendelea kusotea namba katika kikosi cha kwanza.
    Nyota huyo wa Mexico, kupitia ukurasa wake Twitter, ameretweet habari ya Sky Sports kwa wafuasi wake, lakini baadaye akaiondoa posti yake.
    Inahusisha nukuu kutoka kwa mchezaji wa kimataifa wa Mexico, Carlos Vela aliyesema hakutana na hasara yoyote iwapo akiondoka au kubaki Old Trafford.

    Majibu: Haya ndiyo majibu ya Hernandez kuhusu mustakabali wake Manchester United
    Taking off, Javier? Hernandez has been advised to quit the Red Devils
    Unaondoka, Javier? Hernandez ameshauriwa kuondoka kwa Mashetani hao Wekundu
    Floored: Hernandez had scored three in two before being dropped to bench for Saturday's win at Fulham
    Jamvini: Hernandez amefunga mabao matatu katika mechi mbili kabla ya kupigwa benchi Jumamosi kwenye mechi na Fulham 

    "Javier ni rafiki yangu mzuri - na natumaini anapoata nafasi nyingi msimu huu Manchester United," amesema mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, ambaye kwa sasa yupo Real Sociedad na anajianda kuivaa United katika Ligi ya Mabingwa kesho.
    "Ni mmoja wa wamaliziaji wazuri England na anastahili nafasi chini ya kocha mpya. Ikiwa atakuwa anapangwa kila mechi, atafunga, hivyo kwa ujumla sielewi kwa nini mchezaji wa kiwango chake hachezi mechi zaidi,".
    "Kama hapati nafasi ya uhakika ya kucheza, atahitaji kufikiria juu ya kuondoka,".Advice: Former Arsenal forward Carlos Vela believes his Mexico team-mate should leave United if first-team chances continue to be limited
    Ushauri: Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela anaamini mchezaji mwenzake wa Mexico anapaswa kuondoka United ikiwa ataendelea kukosa nafasi ya uhakika ya kucheza

    "Wakati wote anataka kufanikiwa katika klabu kubwa - lakini kama hapewi nafasi huko, kuna timu nyingine England na Ulaya zinamtaka,".
    Hernandez alifuga mabao matatu katika mechi mbili, kabla ya kuwekwa benchi na kuingizwa baadaye katika mechi na Fulham Jumamosi, hata hivyo akashindwa kung'ara akitokea bencghi.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ameifungia mabao 54 United tangu ajiunge nayo mwaka 2010, lakini ametokea benchi mara 38, wakati alianza mara 43 katika Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CARLOS VELA AMTIA NDIMU CHICHARITO, AMUAMBIA; "KAMA MAN UTD HAWAKUPANGI ONDOKA ZAKO, WEWE LULU ULAYA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top