• HABARI MPYA

    Monday, November 04, 2013

    NANI ATAMALIZA KILELENI MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KU BARA, AZAM, MBEYA CITY AU YANGA?

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam

    MECHI ZA MWISHO MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KUU BARA

    Novemba 6, 2013
    JKT Ruvu vs Coastal Union (Azam Complex, Chamazi)
    Ashanti United vs Simba SC (Taifa, Dar es Salaam)
    Kagera Sugar vs Mgambo Shooting (Kaitaba, Bukoba)
    Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar (Mabatini, Mlandizi).
    Novemba 7, 2013
    Azam FC Vs Mbeya City (Azam Complex, Chamazi)
    Yanga Vs Oljoro JKT (Taifa, Dar es Salaam)
    Rhino Rangers Vs Prisons (A.H. Mwinyi, Tabora)
    ANGALAU msimu huu hadi sasa imeshuhudiwa Ligi Kuu yenye ‘kurusha roho’ tofuti na ligi tulizozizoea miaka ya karibuni washindani ni Yanga, Azam na SiImba SC.
    Asante Mbeya City, timu mpya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeongeza ushindani msimu huu, hadi sasa ikiwa inapambana na Azam FC kuwania kumaliza mzunguko wa kwanza kileleni.
    Ni kama wapangaji wa ratiba ya ligi msimu huu ‘waliota’ wakapanga Azam FC imalize mzunguko wa kwanza na Mbeya City- hilo litakuwa bonge la mechi miongoni mwa mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo Novemba 6 na 7 mwaka huu. 
    Kikosi cha Azam FC kinaongoza Ligi Kuu, lakini wakifungwa na Mbeya City wanaweza kupormoka hadi nafasi ya tatu
    Novemba 6 ni JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Ashanti United na Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kagera Sugar na Mgambo Shooting Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na Ruvu Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.
    Na Novemba 7, mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora.
    Yanga SC wapo nafasi ya tatu, lakini inaweza kupanda kileleni Azam na Mbeya City wakitoka hata sare.
    Kwa mazoea hakuna shaka wengi watakwenda Uwanja wa Taifa Novemba 7, kushuhudia mechi kati ya Yanga na Oljoro, lakini kwa maana ya mechi ya kufungia msimu, basi itakuwa Chamazi Azam na Mbeya City.
    Mshindi wa mechi hiyo moja kwa moja atamaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu akiwa kileleni, na atakayefungwa anaweza kuporomoka hadi nafasi ya tatu, iwapo Yanga SC itashinda mechi yake na Ojoro. Wakitoka sare, Azam itabaki juu ya Mbeya City na Yanga inaweza kupanda kileleni ikishinda. 
    Mbeya City inaweza kumaliza kileleni ikiifunga Azam Chamazi
    Timu hizo zina pointi sawa, 26 kila moja, lakini Azam inabarizi kileleni kwa wastani wake mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. 
    Mbeya City na Azam ndizo timu pekee ambazo hadi sasa msimu huu hazijapoteza mechi, wakati mabingwa watetezi, Yanga waliopoteza mechi moja tu mbele ya Azam, wanakaa nafasi ya tatu kwa pointi zao 25. 
    Mechi zote za mwisho zitaanza na kumalizika muda mmoja ili kukwepa upangaji wa matokeo na zitaonyeshwa na Azam Televisheni. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NANI ATAMALIZA KILELENI MZUNGUKO WA KWANZA LIGI KU BARA, AZAM, MBEYA CITY AU YANGA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top