Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KOCHA Mholanzi wa Yanga SC, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, ameondoka jana usiku mjini Dar es Salaam kurejea kwao kwa mapumziko mafupi, lakini wasiwasi ni kwamba alipelekewa Mkataba mpya, akagoma kusaini, akidai una mapungugu urekebishwe kwanza.
Beki wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, amemaliza Mkataba wake tangu Oktoba mwaka jana, lakini uongozi ukaamua kusubiri hadi amalize mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ndipo asaini Mkataba mpya.
Ameahidi kurudi ndani ya wiki moja, lakini wakati huo huo kuna habari kwamba, Brandts ana ofa kutoka klabu nyingine, zikiwemo za hapa nyumbani Tanzania.
Brandts anaiacha Yanga SC ikiwa kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 28, moja zaidi ya Azam FC na Mbeya City zinazofuatia.
Mtaalamu huyo, aliyezaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland, ambaye mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht na De Graafschap alitua Yanga SC Oktoba mwaka jana akitokea APR ya Rwanda.
Brandts aliichezea mechi 28 timu ya taifa ya Uholanzi na kuifungia mabao matano na pia alicheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1978.
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako alifanya kazi hadi mwaka jana alipohamia Jangwani mwaka na Mei mwaka huu akaipa ubingwa wa Bara.

![]() |
| Brandts ameondoka bila kusaini Mkataba mpya Yanga SC |

| Brandts anaiacha Yanga SC kileleni mwa Ligi Kuu |
Katika fainali hizo, Raundi ya pili kwenye mechi na Italia, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifungia mabao timu zote katika mechi moja kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Alianza kujifunga dakika ya 18, kisha akaisawazishia Uholanzi dakika ya 50 katika mechi ambayo, mchezaji mwenzake Arie Haan baadaye aliifungia timu yake bao la ushindi na kutoka kifua mbele kwa mabao 2–1.
Alipostaafu soka akawa kocha na katikati ya msimu wa 2007–2008, Brandts aliambiwa hataongezewa mkataba NAC-Breda, licha ya matokeo mazuri ya kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Uholanzi (Eredivisie), ingawa uamuzi huo haukuwafurahisha mashabiki wa timu hiyo na nafasi yake akapewa Robert Maaskant kuanzia msimu wa 2008–2009.
Akateuliwa kuwa Kocha wa Rah Ahan mwaka 2009, kabla ya kufukuzwa Desemba 2009 na kuibukia APR ya Rwanda mwaka 2010, ambako alifanya kazi hadi mwaka jana alipohamia Jangwani mwaka na Mei mwaka huu akaipa ubingwa wa Bara.

.png)
0 comments:
Post a Comment